Habari za Punde

Wafanyakazi Wizara ya Afya Zanzibar Wafanya Tafrija ya Kuwaaga Waziri Wao na Naibu Waziri.

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo (hawapo pichani) waliofika katika sherehe za kuagwa kwao zilizofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar. Kushoto Waziri wa AfyaZanzibar Mhe. Rashid Seif Suleiman.
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Rashid Seif Suleiman akitoa nasaha zake na kuwashkuru watendaji wake kwa mashirikiano yao katika sherehe za kuagwa kwao zilizofanyika Wizara ya Afya, (kushoto) Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mohammed Jidawi na (kulia) Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo. 
Baadhi ya Mafisa wa Wizara ya Afya Zanzibar wakisikiliza nasaha kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo (hayupo pichani) katika sherehe za kuaaga zilizofanyika Wizara ya Afya.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Mohammed (kushoto) akimkabidhi zawadi Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Rashid Seif Suleiman katika sherehe za kuagwa kwao zilizofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar. 
Wafanyakazi wa Wizara ya Afya Zanzibar wakiitikia dua baada ya kumaliza hafla ya kuwaaga Waziri na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.