Mkalimani wa Lugha za Ishara ambae pia ni mtaalam wa nukta nundu Kisiwani Pemba Ndg. Farid Moh’d akitoa mafunzo ya vitendo kuhusu utumiaji wa kifaa cha kupigia kura (tactile ballot ) kwa watu wenye ulemavu wa Kuona. Mafunzo hayo yalifanyika Chake Chake Tarehe 14/10/2015 katika ukumbi wa Afisi za mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba
Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Ya Zanzibar Mh. Ayoub Bakar Hamad akitoa ufafanuzi kuhusu kifaa cha kupigia kura kwa wasioona,ufafanuzi huo aliutoa tarehe 19/10/2015 katika mafunzo ya watu waioona juu ya matumizi ya kifaa hicho ambayo yaliendeshwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ukumbi wa ECROTANAL Zanzibar.
s

Semina ya Viziwi iliyoendeshwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Tarehe 20/10/2015 Hoteli ya Bwawani Salama Hall, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar iliendesha Mafunzo juu ya utaratibu wa Upigaji Kura kwa makundi yote ya watu wenye Ulemavu ili kutoa Ushiriki Mzuri kwa makundi yote na kila mmoja aweze kuitumia vilivyo haki yake ya kupiga kura.
No comments:
Post a Comment