Habari za Punde

Ajali mbaya ya gari Kibele







Wadau,
Kuna ajali mbaya imetokea mchana huu kwenye saa 8.10 ambayo imemhusisha askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) (jina halikupatikana). 

Mazingira ya ajali hiyo ambayo imetokea katika kijiji cha Kibele, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja ni mwendo kasi wa dereva huyo ambaye alishindwa kuidhibiti gari ndogo aina ya Toyota Spacio yenye namba za usajili Z 511 FG na hatimaye kuacha barabara na kugonga mnazi ambao uliangukia gari na baadae gari kuwaka moto. 

Dereva alitolewa ndani ya gari akiwa amebanwa na air bags zilizofyatuka na kuokoa uhai wake. Alipata majeraha madogo ya kuchubuka kwenye mikono yake iliyokuwa inavuja damu. (Kwa maadili ya taaluma ya habari sikuwaletea picha ya dereva ambaye alikuwa peke yake ndani ya gari hiyo ila gari ni kama inavyoonekana kwenye hizo picha.)

Hassan, Hassan S.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.