Na Haji Nassor, Pemba
TUME ya Ukimwi Zanzibar (ZAC) ofisi ya Pemba, inaendelea kukasirishwa na unyama wa kupewa majina mabaya kama vile ‘wasambaza sumu’ watoto wanaoishi na VUU au wazazi waliokufa kwa tatizo hilo.
ZAC imesema, suala la kuwapachika watoto majina mabaya, huwaongeza wasiwasi wa ugonjwa watoto hao, jambo ambalo halipendezi ndani ya jamii .
Kauli hiyo imetolewa na Afisa kutoka Tume hiyo kisiwani humo Ali Mbarouk Omar, alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, juu ya kuwepo kwa malalamiko kwa wazazi wanaoishi na VUU kwa watoto wao, kupewa majina mabaya.
Ali, alieleza kuwa jambo hilo kamwe sio la kistaarabu, maana hakuna alieomba kuwa na tatizo hilo, na kwamba unyanyapaa huo na mwengine hausaidii kupunguza maambukizi mapya.
Afisa huyo alisema jamii ya leo, imekuwa ikisahau wajibu na jukumu lao katika kupunguza maambukizi mapya ya VUU, na ndio kwanza wanaweka vikwazo kwa wengine, kushindwa kujitangaaza.
Alieleza kuwa, ZAC imekuwa msatari wa mbele kuielimisha jamii juu ya athari za aina zote za unyanyapaa, lakini jamii imekuwa sugu, kubadili tabia na sasa unyanyapaa hadi kuwaelemea watoto.
“Utshangaa kwamba kila mtu anaishi duniani kwa kufauta miongozi ya imani ya dini yake, lakini bado haoni kama ni kosa kuendesha unyanyapaa’’, alisikitika.
Alitaja baadhi ya majina wanayopewa watoto wanaoishi na VUU au ambao wazazi wao wameshafariki kwa tatizo hilo, kuwa ni ‘watembeza sumu’ watoto wa mawaya, wenye wali wetu pamoja na majina ya watoto wa ukimwi.
Hivyo ameiasa jamii kuacha tabia hiyo, ikijua kuwa tatizo hilo linaweza kumfika kila mmoja, bila ya kutarajia, hivyo iwapo kuna unyanyapaa ni kazi kupunguza.
Kwa upande wake Mratibu wa Jumuia ya watu wanaoishi na VVU Pemba, ZAPHA+ Mmanga Seif Massoud anasema kwamba kwa sasa hali imepungua kidogo maana hata idadi ya malalamiko yameshuka.
“Ilikuwa kila mwezi tunapokea lalamiko moja, la wazazi kwa watoto wao kupewa majina mabaya, lakini sasa tumeshakaa hadi mwezi hakuna kesi, kidogo ahuweni ipo’’,alisema.
Hata hivyo alisema juhudi za kutoa elimu ni sababu moja wapo ya kupungua kwa hali hiyo, ingawa amesema wanaendelea kuwaelimisha wananchi
Nae Juma Hamad Haji wa Msuka wilaya ya Micheweni, alisema yeye mwanawe ambae amezaliwa akiwa hana maambukizi, amekuwa akimbuna na kupewa majina mabaya.
“Yeye tumemzaa hana maambukizi na jamii inajua lakini huitwa mtoto wa ukimwi au wengine humuita kifo kifo, sasa haya hayasaidii kupunguza maambukizi mpaya’’,alisema.
Nae Mariyam Said Abdalla amabe ameolewa na mwanamme ambae hana maambukizi mkaazi wa Wawi, alisema awali unyanyapaa ulikuwa zaidi kwao, ingawa kwa sasa hilo limehamia kwa watoto wao.
Anasema alifanya juhudi kubwa ya kuelimisha jamii kwenye eneo analoishi hadi skuli ya Michakaini anayosomwa mwanawe, ambpo kwa sasa hali inavutia wastani
“Sisi wameshatuona kwamba hatunyanyapaliki tena, sasa watoto wetu walioskulini na vyuoni ndio wananyanyapaliwa na hata baadhi ya walimu wao wasio na elimu’’,alisema.
Mmoja katia ya wazazi ambae hana maambukizi wala mwanawe, Kassim Juma Omar, alisema bado jamii inadhana kwamba kila aliepata maabukizi sio mtiifu.
“Watu hawataki kufahamu kuwa Ukimwi au Viruisi, sio kila alienavyo kwamba amefanya njia chafu, wengine kwa bahati mbaya, na kila mmoja anaweza kupitikiwa’’,alisema.
Kwa upande wake Mayasa Habibu wa Machomane alisema, ni vyema kwa sheria ya mambo ya ukimwi, ikaharakishwa ili kuwaadhibu wanaoendesha vitendo vya unyanyapaa .
No comments:
Post a Comment