Jumuiya ya Wazanzibari waishio Sweden Scandinavia (ZANDIA) inawatakia wa Zanzibar na wadau wote wanaoitakia Zanzibar neema kheri ya mwaka mpya 2016, Mwenyezi Mungu ijalie nchi yetu amani, upendo, na ushikamano kwa Wazanzibari wote ulimwenguni.
Tunajenga imani kubwa kuwa kuna mwelekeo wa kupatikana muafaka kwenye vikao vinavyoendelea kila siku huko nyumbani, na kuiweka nchi yetu katika Amani na utulivu, ili kupatikana Rais aliechaguliwa kihalali katika nchi yetu tuipendayo Zanzibar.
Mungu Ibariki Zanzibar na waZanzibari wote Ameen
No comments:
Post a Comment