Habari za Punde

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Afungua Mafunzo ya Awali kwa Watumishi wa Idara ya Wakimbizi leo Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak 

Abdulwakil akizungumza  na washiriki  wa Mafunzo ya awali kwa 

Watumishi wa Mkataba wa Idara ya Huduma kwa 

Wakimbizi(hawapo pichani),wakati alipofungua mafunzo hayo 

yenye lengo la kuwajengea uwezo watumishi wapya, katika 

ukumbi wa mikutano wizarani hapo,jijini Dar es Salaam.Kulia ni  

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Numbilya Mpolo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak 

Abdulwakil akizungumza  na washiriki  wa Mafunzo ya awali kwa 

Watumishi wa Mkataba wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi 

wakati alipofungua mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea 

uwezo watumishi wapya, katika ukumbi wa mikutano wa wizara, 

jijini Dar es Salaam.Kulia ni  Kaimu Mkurugenzi Idara ya 

Huduma kwa Wakimbizi, Numbilya Mpolo, kushoto ni 

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa  Rasilimali 

Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa .
Washiriki wa Mafunzo ya awali kwa Watumishi wa Mkataba wa 

Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa 

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil(hayupo 

pichani), wakati alipofungua mafunzo hayo katika ukumbi wa 

mikutano wizarani hapo,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa  Rasilimali 

Watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa, 

akizungumza na washiriki wa Mafunzo ya awali kwa Watumishi 

wa Mkataba wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi(hawapo 

pichani),kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Utawala 

na Usimamizi wa Idara ya Wakimbizi, Deusdedit Masusu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak 

Abdulwakil(watatu kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja 

na washiriki wa Mafunzo ya awali kwa Watumishi wa Mkataba wa 

Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, muda mfupi baada ya kufungua 

mafunzo hayo katika ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam 

wanne kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na 

Usimamizi wa  Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa na 

wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi  wa Idara ya Huduma kwa 

Wakimbizi, Numbilya Mpolo.

(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,MOHA)

Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.