Habari za Punde

Matukio ya Picha Mitaani Zenj

Gari za kubebea mizingo zikiwa zimeegeshwa kando ya barabara zikisubiri wateja wakati wa kuingia kwa meli ili kuweza kupata mizigo, uegeshwaji wa magari kama hivi, Mamlaka ya Mji Mkongwe wakilifanyika kazi suala hili kwa maegesho ya aina hiyo na kuwa usumbufu kwa wananchi wengine wanaotembelea mji mkongwe. 

Askari wa Polisi Jamii katika Mji Mkongwe wa Zanzibar akimtaka dereva wa gari hiyo kuondoa gari yake ambayo imeegeshwa katika eneo halistahili kuegesha katika katika maeneo ya malindi ili kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo wakati wa kufika kwa male eneo hilo huwa na msongamano mkubwa wa magari.
Wachuuzi wa Samaki wakiwa katika ufukwe wa pwani ya Malindi Zenj wakisubiri wavuvi kurudi ili kuapa ta bidhaa hiyo ya samaki, katika kipindi hichi cha upepo samaki wamekuwa haba katika soko hilo la malindi na kufikia mtungo mmoja wa masaki katika mnada hapo hufikia kati ya shilingi 50,000 inategemea ukubwa wa samaki.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.