TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
UTANGULIZI;
Habari za Asubuhi
ndugu zangu wana habari,
Leo tarehe 17/01/2016,Mimi Bonnah
M.Kaluwa ambaye ni mbunge wa jimbo la Segerea katika wilaya ya Ilala.
Nimekuiteni Asubuhi ya leo ili
kuwashirikisha katika uzinduzi wetu wa kampeni
ya MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA ndani ya jimbo la Segerea,kwakujua dhahiri kuwa ushiriki wa wana habari ni
muhimu sana katika kufanikisha kampeni hii kwa ajili ya maendeleo ya elimu katika
jimbo la Segerea na nchi kwa ujumla .
MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA ,ni kampeni isiyo na malengo ya
kumnufaisha mtu binafsi bali inalenga kuisaidia jamii ndani ya jimbo la Segerea
katika upatikanaji wa elimu bora kupitia maboresho ya miundombinu
ya shule kama madarasa, vyoo,
mifumo ya maji safi na salama,
madawati na kadhalika.
Ndugu zangu ninyi wote ni
mashahidi kuwa zipo changamoto nyingi katika sekta ya elimu ndani ya nchi yetu
zinazohusiana moja kwa moja na masuala
niliyoyataja hapo juu.Huku tukilenga kupata;
•madawati 15,000,
•matundu ya vyoo vya kisasa 1335,
•visima vya maji 12, na
•vyumba maalum vya watoto wa kike 38.
Kimsingi kampeni hii ni
muendelezo wa kampeni iliyowahi kufanyika katika kata ya KIPAWA [ndani ya
jimbo la Segerea] kwa kusimamiwa na mfuko wangu
wa elimu uitwao BONNAH EDUCATION TRUST FUND mnamo
mwaka 2011,kipindi nilipokuwa diwani wa kata hiyo.Kwakuzingatia mafanikio na matokeo chanya ya kampeni hii
katika ngazi ya kata;
Kwa moyo wa dhati kabisa,
kwakuwa nimechaguliwa kuwa mbunge wa
jimbo la Segerea ,nimedhamiria kupeleka mafanikio ya kampeni hii kwa kushirikiana na mfuko wangu wa BONNAH
EDUCATION TRUST FUND katika ngazi ya jimbo ili basi kila mwananchi ndani ya
jimbo la Segerea anufaike na kampeni
hii.
Ili kufanikisha kampeni hii,
tutawashirikisha wadau mbalimbali wa elimu waliopo ndani na nje ya jimbo la
Segerea kama vile Serikali, Makampuni, Mashirika na watu binafsi.
Kampeni ya MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA tunatarajia kuifanya kwa awamu mbili
ambazo ni;
¡. Matembezi ya
hiyari (Charity walk) na
¡¡.
Chakula cha jioni (Gala dinner).
MATEMBEZI YA HIYARI.
Matembezi haya yatafanyika ndani
ya jimbo kwa kushirikisha wananchi ,na wadau wote wa elimu tukiwa na lengo moja
tu la kukusanya fedha za kuboresha miundombinu ya elimu katika jimbo letu la
Segerea kwa shule za msingi katika kata
zote kumi na tatu[13] za jimbo la Segerea.
Matembezi haya yanatarajiwa
kufanyika tarehe 25/02/2016, kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 10 alasiri.
CHAKULA CHA JIONI
Awamu hii ya pili na ya mwisho ya
kampeni yetu inatarajiwa kufanyika tarehe 03/06/2016 kuanzia saa 2 usiku na kuendelea.
Katika awamu hii tunatarajia kuwa
na chakula cha jioni cha pamoja ambapo wageni kutoka maeneo mbali mbali na nje
ya nchi watashiriki nasi katika kuchangia na kuhamasisha upatikanaji wa
fedha na mahitaji yote muhimu kuelekea
ufanikishaji wa kampeni yetu.
Tunawashukuru ninyi waandishi wa
habari na wageni wote waalikwa kwa
kushiriki nasi katika uzinduzi huu wa kampeni
hii ya MAZINGIRA BORA KWA ELIMU
BORA jimbo la Segerea.
Hivyo natangaza rasmi kuwa kampeni hii imezinduliwa rasmi leo tarehe 17/01/2016.
Ahsanteni sana
Mawasiliano
Mh.Bonnah Kaluwa ; 0758
324 552
Bi. Jackline; 0713
711 632
Bw.Shamsudin; 0713 754 869
No comments:
Post a Comment