Mwanasaikolojia Anti Sadaka amewafunda wanawake wa Zanzibar wanaoshiriki mafunzo ya ujasiriamali ya kujikita katika biashara ya Vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yanaendeshwa na wataalamu kutoka taasisi ya Manjano Foundation na Zanzibar Chamber of Commerce yanayoendelea Zanzibar kwa wiki nzima.
Anti Sadaka amewataka wanawake hao kujitambua kwa lengo la kufikia malengo yao waliojiwekea. Akieleza zaidi katika semina hiyo amewataka wanawake hao kujitambua wao ni nani wana nafasi gani kwenye jamii inayowazunguka, kufanya kazi kwa bidii na kudumisha nidhamu yao kwa kila wakifanyacho kwa lengo la kufikia malengo yao.Pia amewaasa wanawake walioshiriki mafunzo hayo mjini Zanzibar kuchangamkia FURSA zinazowazunguka.
Semina hiyo inawanufaisha wanawake wa Zanzibar kwa lengo la kuwaongezea kipato na pia kuweza kujiajiri ili kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira.
Anti Sadaka amewashauri wanawake wasiache kujifunza na kujibweteka baada ya mafunzo haya kuisha isipokuwa wawe makini kutafuta elimu zaidi ya kujiongezea ujuzi katika kazi zao.
No comments:
Post a Comment