Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mhe. Balozi Simon Sirro amesema kuwa jiografia ya Kigoma inayopakana na Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, inaifanya mkoa huo kuwa na nafasi nyeti katika kudumisha amani. Akisisitiza kuwa amani si hiari bali ni sharti la msingi kwa ustawi wa wananchi.
Na Fredy Mgunda,Kigoma.

Balozi Sirro ametoa kauli hiyo, wakati wa Kongamano la kuliombea taifa Amani katika Uchaguzi Mkuu 2025 lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Kasulu (TCC), lililoandaliwa na Kamati ya Maridhiano kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu.
“Bila amani, biashara ya mipakani haiwezi kustawi, wananchi hawawezi kuendeleza shughuli zao za kilimo, uvuvi na biashara ndogo ndogo. Amani ndiyo uti wa mgongo wa maendeleo ya Kigoma na Tanzania kwa ujumla,” amesema.
Ameongeza kuwa viongozi wa dini wanapaswa kuepuka kutumia nyumba za ibada kama majukwaa ya kisiasa, kwani kuchanganya masuala ya dini na siasa kunaweza kuhatarisha mshikamano wa kijamii.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Mhe. Kanali Isaac Mwakisu, amewashukuru viongozi wa dini kwa kushirikiana na serikali katika matukio mbalimbali na kuwataka waendelee kuwaombea viongozi ili watoe maamuzi yenye busara kwa wananchi.
Naye Katibu wa Kamati ya Maridhiano Wilaya ya Kasulu Sheikh Nasib Rajab kutoka dhehebu la SHIA, amesema kongamano hilo limeonesha mshikamano wa wananchi licha ya tofauti za kiitikadi, jambo linalosaidia kuimarisha umoja na mshikamanano.
Vilevile, Askofu wa Kanisa la FPCT Jimbo la Kasulu, Shadrack Bunono, alibainisha kuwa mtu anayekalia kiti cha mamlaka anapaswa kutumia busara na hekima katika maamuzi yake kwa manufaa ya wananchi, na kusisitiza kuwa sala na maombi kwa viongozi ni msingi wa mafanikio katika wilaya hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mhe. Balozi Simon Sirro amesema kuwa jiografia ya Kigoma inayopakana na Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, inaifanya mkoa huo kuwa na nafasi nyeti katika kudumisha amani. Akisisitiza kuwa amani si hiari bali ni sharti la msingi kwa ustawi wa wananchi.
No comments:
Post a Comment