Habari za Punde

Queen Julieth Lugembe wa ACT-Wazalendo Azindua Kampeni Manzese

 

Dar es Salaam – Wananchi wa Ubungo pamoja na wafuasi wa Chama cha ACT Wazalendo wamejitokeza kwa wingi leo katika viwanja vya Manzese Bakresa, kushuhudia uzinduzi wa kampeni za ubunge wa mgombea wa Jimbo la Ubungo, Queen Julieth Lugembe.

Uzinduzi huu umempa nafasi Queen Julieth kuzungumza moja kwa moja na wananchi wa jimbo hilo, akieleza ahadi zake na mipango yake ya maendeleo endapo atapata nafasi ya kuliongoza Jimbo la Ubungo baada ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

Wanachama wa ACT Wazalendo na wakazi wa Ubungo wameonyesha mshikamano na hamasa kubwa, wakisisitiza umuhimu wa kuleta mabadiliko na maendeleo kupitia sera na dhamira ya mgombea wao.






No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.