WAGOMBEA Uwakilishi na Udiwani wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Jimbo la Magomeni Zanzibar, wakipitia fomu za Uteuzi baada ya kukabidhiwa
na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Ndg.
Khamis Juma Haji, akitowa maelezi ya ujazaji wa fomu hizo, wakati wa hafla hiyo
iliyofanyika katika Ofisi za Uchaguzi Wilaya ya Mjini Unguja Maisara Jijini
Zanzibar leo 3-9-2025.na (kutoka kushoto) Mgombea Uwakilishi Jimbo la Magomeni
Mhe.Mahfuodh Abdallah Mohammed na (kulia kwake) Mgombea Udiwani Wadi ya
Magomeni Mhe.Husna Maulid Mwita na Mgombea Udiwani Wadi ya Sogea Mhe. Mohammed
Said Mohammed.
MSIMAMIZI Msaidizi wa Uchaguzi Ndg.Khamis Juma Haji
akimkabidhi fomu ya Uteuzi Mgombea Uwakilishi Jimbo la Magomeni kwa Tiketi ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe.Mahmoudh Abdallah Mohammed,hafla hiyo
iliyofanyika katika Ofisi za Uchaguzi Wilaya ya Mjini Unguja Maisara Jijini
Zanzibar leo 3-9-2025.
MSIMAMIZI Msaidizi wa Uchaguzi Ndg.Khamis Juma Haji
akimkabidhi fomu ya Uteuzi Mgombea wa Udiwani Wadi ya Sogea kwa tiketi ya Chana
Cha Mapinduzi (CCM) Mhe.Mohammed Said Mohammed,hafla hiyo iliyofanyika katika
Ofisi za Uchaguzi Wilaya ya Mjini Unguja Maisara Jijini Zanzibar leo 3-9-2025.
No comments:
Post a Comment