Mkurugenzi wa Idara ya Utumishi na Uendeshaji katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Rashid Hamdu Makame amesema Serikali itaendelea kuweka Ustawi Bora kwa Wafanyakazi wakati na baada ya Utumishi.
Ameyasema hayo wakati akifungua Mafunzo ya kuelewa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo huko Ukumbi wa Wizara hiyo Migombani Migombani Wilaya ya Mjini.
Amesema lengo ni kuwawezesha Wafanyakazi hao, kuweza kujikimu katika kipindi cha kumalizika Utumishi wao Serikalini.
Amesema Serikali, inahakikisha Wafanyakazi wote wanaingiziwa Michango katika Mfuko wa ZSSF ili waweze kujipatia kipato wakati watakapomaliza muda wa Utumishi Serikalini.
Nae Afisa Uhusiano, Elimu kwa Umma kutoka Mfuko wa ZSSF Riziki Stanly amewataka Wanachama wa Mfuko huo, kufuatilia michango wanayotoa ili kuepuka kasoro zinazojitokeza wakati wanapodai mafao yao ya kustaafu.
Aidha amesema Wanachama hao, wanatakiwa kujua kiasi cha michango walioweka, kupatiwa Vitambulisho vya Uanachama pamoja na mafao ya kiinua mgongo na Pencheni.
Kwa Upande wake Afisa Mfuko wa Hiari kutoka ZSSF Mohamed Hussein amesema Mfuko huo, unawalenga wafanyakazi wa Sekta isiokuwa rasmi kama vile Wakulima, Wavuvi, Wafugaji, Makuli, Wajasiriamali na Wanafunzi.
No comments:
Post a Comment