Habari za Punde

Wasira:Tunamuombea kura rais dk.samia lakini Watanzania ni mashahidi wa kazi aliyoifanya

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ( Bara) Ndg Stephen Wasira akizungumza na Viongozi na Wanachama  akiwa katika Muendelezo wa ziara yake ya kukutana na Viongozi pamoja na Wagombea wa  CCM Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara , Kuelekea katika  Uchaguzi Mkuu Mwaka 2025  tarehe 02 Septemba, 2025.

Na Mwandishi Wetu,Babati

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira amesema wakati wanamuombeq kura mgombea urais kwa tiketi ya Chama hicho Rais  Dk.Samia Suluhu Hassan Watanzania ni mashahidi wa kazi kubwa aliyoifanya katika miaka minne na nusu ya uongozi wake.

Akizungumza leo Septemba 1,2025 latika kikao cha ndani kilichohusisha viongozi na wana CCM Wilaya ya Babati Wasira amesema kwa kuwa tangu Rais Samia amechukua uongozi kutoka kwa mtangulizi Hayati Dk.John Mafuli kuna mambo makubwa yamefanyika nchini.

"Wanataka kumuondoa lakini sababu hawana na ukisema nao wapinzani pembeni wanasema lakini nyie wakubwa ,mmefanya mambo mengi.Nilikuwa  mjumbe wa Kamati iliyoandika Ilani mpya ya mwaka 2025-2030 akanipigia kiongozi mmoja wa chama cha upinzani anasema nimeisoma Ilani yenu mmeandika kila kitu sasa sisi tutaandika nini?

"Kwasababu CCM tulikuwa na Ilani ya Uchaguzi Mkuu  2020  imetekelezwa mpaka tumevuka mpaka na ushahidi wake hata hapa Babati upo katika sekta zinazohusu watu.Tumejenga zahanati 19 , vituo vya afya 8 , tumejenga hospitali mbili moja ya kukarabati lakini kama imejengwa upya.

"Najua kuna tatizo  la maji hapa  lakini tumeikabidhi mamlaka ya maji ili kutatua changamoto hiyo.Kwahiyo nakuja kuwaambia tumetekeleza sana Ilani  na kwahiyo tunapokuja kuomba kura ya Rais Dk.Samia Suluhu Hasan Watanzania ni mashahidi wa mambo makubwa yaliyofanyika katika kipindi cha miaka minne na nusu ya uongozi wake,"amesema Wasira

Amepngeza wakati tunafikiwa miaka minne na nusu iliyopita kutokana na kifo cha Rais Hayati Dk,John Magufuli alimuachia Rais Dk.Samia kazi za kufanya alizozianzisha  na wakati ule kulikuwa na hofu wanasema mwanamama huyu ataweza.

Amefafanua kwani wanaume wameshazoea mfumo dume mpaka urais wanauhusisha na mfumo dume utafikiri kila mwanaume anaweza kuwa Rais.Hofu nyingine ilikuwa inajengwa tu na nyingine ni ya mazoea lakini Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kazi aliyoachiwa akaweka maneno mawili anakwambia Kazi Iendelee.

"Aliachiwa bwawa la mwalimu Nyerere ujenzi na bwawa lile ujenzi umekamilika na mitambo yote tisa imewashwa,pia aliachiwa ujenzi wa reli ya SGR ambayo Dar es Salaam hadi Dodoma inatoa huduma ujenzi unaendelea wa reli hiyo.

'' Na sisi Tanzania tunataka kuthibitishia Dunia, kwamba kwanza sisi tunaamini patika usawa wa binaadamu na binadamu sote ni sawa wakiwemo kina mama, kwaiyo chama chetu ambacho kikubwa kimemuweka  Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti tiketi, kazi ya chama chetu ni kuuza tikrti ambayo inaongozwa na Mwana mama na kuhakikisha anashinda tena kwa kura nyingi''.
Mwisho

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.