Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dk. Hamisi Kigwangalla (aliyekaa) akiwa katika ibada maalum ya kuombea wagonjwa duniani iliyofanyika leo katika Hospitali ya Ndala,Nzega Mkoani Tabora. Wengine kulia ni Rudrovic Mwananzila na kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Jacqueline Liana.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dk. Hamisi Kigwangalla amesema kwamba wao kama viongozi wataendelea kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli kutumbua majibu yanayokwamisha kutokupatikana kwa huduma bora za afya, bila kuogopa wala kumwonea mtu kwa ajili ya maslahi ya taifa.
Aidha Dkt. Kigwangalla alisema watafanya hivyo kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu ili kuhakikisha kila mtu anatimiza wajibu ipasavyo.
Dk.Kigwangalla ameyasema hayo leo 11 Februari wakati wa maadhimisho ya 24 ya ibada maalum ya kuwaombea wagonjwa Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika jimbo kuu la Tabora na baadae kwenye Hospitali ya Ndala, iliyopo Kata ya Ndala, Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora.
“Tutaendelea kutumbua majibu bila ya kmwonea mtu kwa kuwa tunafanya hivyo kwa kuangalia sheria, kanuni na taratibu. Haiwezekani mtu akaiba dawa ambazo zinawasaidia wananchi masikini, halafu sisi tukamwaangalia tu,” alisema Dkt.Kigwangalla.
Alisema majipu hayo yatatumbuliwa kwa watendaji ambao watakaozembea, wasio waadilifu na wasiowajibika katika sekta hiyo ya afya.
Aliongeza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano itakuwa inafanya kazi kwa kuwafuata wananchi hususani wanyonge (masikini) mahali walipo ili kuhakikisha baada ya miaka kumi ijayo Tanzania itakuwa na maendeleo ya kiwango cha juu.
Naibu Waziri huyo aliwaomba viongozi wa dini kuendelea kuwaombea kwa kuwa kazi ya kutumbua majibu si rahisi.
Aliuomba uongozi wa hospitali hiyo kuboresha mfumo wa ukusanyaji mapato kwa kutumia njia ya ki-elekroniki kwa sababu umeonyesha matokeo chanya katika hospitali nyinigine.
Akizungumzia kuhusu suala la upungufu wa bajeti, Dkt. Kigwangalla alisema ni vema viongozi hao wadini, asasi za kijamii na taasisi zisizo za kiserikali zinazotoa huduma za afya kutafuta vyanzo mbadala vya kuongeza fedha za kuboresha huduma hizo, kwa kuwa si sekta hiyo pekee yenye changamoto hiyo.
Pia vipaumbele vya shughuli mbalimbali za kuwaletea maendeleo wananchi viko vingi, wakati rasimali fedha haitoshelezi.
Aliwataka uongozi wa hospitali hiyo na nyinginezo za mashirika ya hiari kuwasilisha taarifa za (data cleaning) UTUMISHI ikiwa ni pamoja na kuorodhesha watumishi wanaotakiwa kuondolewa kwenye malipo ya mshahara ili waweze kupatiwa kibali cha kuajiri kwani bila kufanya hivyo kibali hakitaweza kutolewa.
Dkt. Kigwangalla aliongeza kwamba hivi sasa wizara yake iko katika mchakato wa kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma za matibabu za kwa kutumia mifuko ya bima ya afya.
Maadhimisho hayo ni ya kila mwaka ya siku 11 Februari, Wakristo wote wanafanya sala maalum ya kuwaombea wagonjwa wanaosumbuka na maradhi na kuwaombea wapone haraka huku wakiyapokea mateso hayo na kuyaunganisha na mateso ya kristo na kanisa lake hii ni pamoja na kuwaombea ndugu wa wagonjwa katika kuwasaidia wagonjwa wao wakati wa kuwauguza.
Maadhimisho hayo yanaenda sambamba pamoja na kuwahudumia na kutoa misasada mbalimbali.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ludocivk Mwananzila aliwataka Watanzania kuwa na tabia ya kuwatembelea wagonjwa na wafungwa ili waweze kupata faraja.
Kihistoria, Hospitali hiyo ya Ndala, ilianza miaka ya 1930 kama Zahanati ndogo chini ya Masista Wamissionary wa Afrika (Missionary of Our Lady of Afrika-White Sisters) katika jimbo kuu hilo la Tabora
Mwaka 1963 ilikuja kuwa Hospitali kamili huku ikianza na vitanda 115 na wauguzi 15 na daktari mmoja, hata hivyo hadi sasa ina jumla ya vitanda 152, wafanyakaz 125 huku wakiweza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje wapatao 38,917 na wagonjwa wa kulazwa 8,428.
Hospitali hiyo baadae ikapandishwa ngazi ya Hospitali huku ikiwa na vitanda 152 huku ikiwa na madaktari mbalimbali.
Wakitoa shukrani zao ni pamoja na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya kwa kuweza kushirikiana bega kwa bega ikiwemo kutoa ruzuku kwa baadhi ya watumishi, posho za watumishi, vitanda vulivyohainishwa, madawa, mafunzo ya watumishi, na mambo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment