Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein Mgeni Rasmin Siku ya Sheria Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu (kulia) na Jiji Mkuu Tanzania  Mohammmed Chande Othman wakati alipowasili viwanja vya Victoria Garden katika sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar
Kikundi cha sanaa na maigizo cha Blackroot walipotoa igizo lao leo katika sherehe zakilele cha siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja mbele ya mgeni rasmi Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe.Said Hassan Saidi akitoa maelezo mafupi na kumkaribisha jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman  Makungu wakati wa sherehe za kilele cha siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar kabla ya kumkaribisha Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na wananchi katika sherehe za siku hii ya sheria
Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akionesha kitabu cha Sheria ya mwaka Zanzibar (ZANZIBAR YEARBOOKOF LAW) Volume 4 baada ya kukizindua rasmi leo katika  sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja,(kulia)Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,(kushoto) naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Ali Abdalla,Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Othman Chande
 Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake leo kwa Wananchi katika sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar zilizofanyika  katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja,(kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Othman Chande
Mwanasheria Mkuu zanzibar Said Hassan Saidi akitoa maelezo mafupi na kumkaribisha jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman  Makungu wakati wa sherehe za kilele cha siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja,{Picha na Ikulu.]

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.