Habari za Punde

Dk Shein Amuapisha Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Ikulu Leo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe Said Hassan Said.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said akiwasili katika Ikulu ya Zanzibar tayari kwa hafla kuapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Ikulu Zanzibar leo 26-3-2016.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg Khamis Mussa wakiingia katika Ukumbi wa Ikulu kwa ajili ya hafla ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar leo asubuhi.
Washauri wa Rais wa Zanzibar Mhe Burhan Sadaat na Balozi Mohammed Ramia wakihudhuria hafla ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Said Hassan Said Ikulu Zanzibar leo.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Abdalla Mwinyi Khamis (katikati) kushoto Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu na Meya wa Mji wa Zanzibar Mhe. Khatib Abrahaman Khati wakihudhuria hafla hiyo ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Ikulu Zanzibar.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Said Hassan Said,akipitia hati ya kiapo kabla ya kuaza kwa hafla hiyo Ikulu leo.
Mkurugenzi wa Mashtaka  Zanzibar Nd,Ibrahim Mzee na Mrajis wa Mahkama Kuu Zanzibar George Kazi ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said leo Ikulu Mjini Unguja
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar Ndg Asaa, akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg Khamis Mussa wakati wa hafla ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Ikulu Zanzibar. 
Familia ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa Ikulu wakati wa hafla ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.Ikulu leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasili katika Ukumbi wa Ikulu kwa ajili ya hafla ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar baada ya kumtangaza jana Mhe Said Hassan Said, Hafla hiyo imefanyika leo Ikulu Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said Ikulu Zanzibar leo asubuhi. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimuapisha Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said Ikulu Zanzibar leo kushoto Katibu Mkuu Kiongozi Dk Abdulhamid Yahya Mzee.Hafla hiyo imefanyika leo Ikulu Zanzibar.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said, akila kiapo Ikulu leo Zanzibar.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisaini hati ya Kiapo ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar baada ya kumuapisha Ikulu leo Zanzibar.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said akitia saini hati yake ya Kiapo baada ya kuapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein. Ikulu leo Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimpongeza Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said baada ya kumuapisha leo Ikulu Zanzibar. 
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar akipongezwa na Mtoto wake baada ya kuapishwa leo asubuhi Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said baada ya kumalizika hafla ya kumuapisha leo asubuhi Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said, na familia yake baada ya kumalizika hafla ya kumuapisha leo asubuhi Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali na Dini waliohudhuria hafla ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Ikulu Zanzibar leo asubuhi.
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu akibadilisha mawazo na Mwenasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said baada ya kuapishwa leo Ikulu Zanzibar.

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Afisi ya Rais Ikulu Zanzibar na Familia yake baada ya kuapicha leo asubuhi Ikulu Zanzibar.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan Said akiwa na Mkewe na Watoto wake katika picha ya pamoja baada ya hafla ya kuapishwa Ikulu Zanzibar leo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.