Na Mwandishi Maalum, New York
Jumuiya ya Kimataifa
imezitaka pande zinazopinga
Nchi Burundi, kumpatia
ushirikiano wa kutosha ,Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin
William Mkapa ambaye ameteuliwa na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kuratibu majadiliano ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchi humo.
Pamoja na pande zinazopingana kutakiwa kufanya hivyo
kwa moyo mmoja, pia Taasisi za Kimataifa na Kikanda ukiwamo Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika,
pamoja na wadau wengine wametakiwa pia kumuunga mkono na kutoa ushirikiano kwa
Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.
Wito huo umetolewa siku ya
Jumatano, hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,
wakati Wajumbe wa Burundi
Configuration walipokutana katika
kikao chao na kujadili hali ya kisiasa
na kiusalama inavyoendelea nchi Burundi kufuatia ziara iliyofanywa na Mwakilisji wa Kidumu wa…… Balozi Jurg Lauber ambaye ni Mwenyekiti wa Burundi Configuration.
“Tunakaribia uteuzi wa Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin
Mkapa kuwa mratibu wa mazungumzo ya
kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro wa kisiasa nchini Burundi.
Tunatoa wito kwa pande zinazopingana nchi
humo, serikali na vyama vya kiasa
kumpatia ushirikiano bila ya mashari yoyote” akasema Mwakilishi wa Marekani.
Naye Mwakilishi wa Kudumu wa
Ubeligiji, Balozi Benedicte Frankinet. Pamoja na kueleza kwamba ujumbe wake
unawasiwasi kuhusu taarifa za kuendelea kwa matukio ya ukiukwaji
wa haki za binadamu na mbinyo kwa vyombo vya habari na uhuru wa watu kutembea.
Amesema .“ Rais Mstaafu wa
Tanzania , Benjamin Mkapa, anauzoefu mkubwa na wa hali ya juu katika uratibu na
utafutaji ufumbuzi wa migogoro ya
kisiasa, ujumbe wangu unakaribisha uteuzi wake, hapana shaka ataratibu na kusimamia
majadiliano jumuishi
yatakayohusisha wadau wote wanaopingana
nchini Burundi wakiwamo pia wajumbe wa asasi zisizo za kiserikali”.
Kwa upande wake,
Mwakilishi wa Kudumu wa Netherland,
Balozi Karel Van Oosterom, amesema ujumbe wake pia unakaribisha uteuzi wa Rais Mkapa, na kwamba pande zinazopinga
nchini Burundi zinatakiwa kuitumia fursa
ya uteuzi wa Mkapa kurejea katika meza
ya majadiliano ambayo yatakuwa
jumuishi na huku akizisihi pande
hizo kutotoa masharti ya aina yoyote ile.
Naye Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Rwanda, pamoja na
kukaribisha uteuzi wa Rais
Mstaafu Mkapa ambaye amesema ana uzoefu mkubwa na wanaimani naye, alimshukuru pia, Rais John Pombe Magufuli
kwa kumteua Mkapa.
Karibu wajumbe wote
waliochangia majadiliano kuhusu hali
ya Burundi walikaribisha na kupongeza
uteuzi wa Mkapa huku, Mjumbe wa Nigeria
pamoja naye kuunga mkono uteuzi wa
Mkapa. Alisisitiza pia kwamba
Majadiliano jumuishi ya kutafuta ufumbuzi wa
kudumu nchini Burundi yanapashwa kumilikiwa na Warundi wenyewe.
Akatahadharisha kwa kusema
kwamba, mashinikizo kutoka nje ya
Burundi hayana nafasi katika
mchakato huo na kwamba hali hiyo
ikiruhusiwa inaweza siyo tu kuathiri
majadiliano hayo lakini pia itakuwa ni
kuwaingilia wananchi wa Burundi.
Mwakilishi wa
Kudumu wa Tanzania, Balozi Tuvako
Manongi akichangia majadiliano hayo,
yeye ametaka ushughulikiaji wa hali tete
ya kisiasa na kiusalama uende sambamba na
uondoajji wa vikwazo vya
kiuchumi kwa Serikali ya Burundi.
“ Hakuna
matinki ya kutia msisitizo wa
kuitaka serikali ya Burundi
kutekeleza mambo kadha wa kadhaa yakiwamo ya
ukiukwaji wa haki za binadamu, pasi kuzungumzia hali mbaya
ya uchumi na kijamii inayoikabili
Burundi na watu wake. Akasema Baloz
i
Nakusisitiza . “Tunapojadili
hali ya usalama tujadili basi na uondoaji wa vikwazo vya
kiuchumi kwa sababu mambo haya yanakwenda kwa pamoja. Njia sahihi ya kusaidia mchakato wa
kutafuta amani ya kudumu nchini
Burundi ni kwa sisi sote tulio katika meza hii kufanya kazi
kwa pamoja na
katika namna inayoeleweka”.
Vile vile Balozi Manongi
ambaye Tanzania ni mjumbe wa Burundi Configuration ambayo ni sehemu
ya Kamisheni ya Ujenzi wa Amani ( Peace
Building Commission) amesisisiza wananchi wa Burundi kumiliki mchakato wa majadiliano kuhusu mustakabali wa
nchi yao.
Hoja ya kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi, Warundi kumiliki majadiliano yao,
pia imeungwa mkono na
mjumbe wa China ambaye amesema
Haki za binadamu zinahusu pia haki ya
kupata maendeleo na kwamba Jumuiya ya Kimataifa inatakiwa kuisadia Burundi
kiuchumi ili wananchi wapate maendeleo
ambayo ni haki yao.
No comments:
Post a Comment