Habari za Punde

Star Times yamleta nchini mchezaji Kanu kutoka Nigeria kuzindua duka jengo la Mkuki Mall

 Mchezaji wa zamani wa Nigeria, Nwankwo Kanu akizungumza na wanahabari baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jana usiku kwa mwaliko wa siku tano wa Kampuni ya Vizimbuzi ya StarTimes.
 Mchezaji wa zamani wa Nigeria, Nwankwo Kanu alipokuwa akiwasili Uwanja wa Ndege.
 Hapa Kanu akihojiwa na wanahabari. Kushoto na kulia ni Mabaunsa waliokuwa wakimlinda baada ya kufika Uwanja wa Ndege kabla ya kuelekea Hoteli ya Serena.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Be. Lanfang Liao (kulia), akimuelekeza jambo mchezaji huyo wakati wakielekea kupanda gari kuelekea Hoteli ya Serena. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa StarTimes Tanzania,  William Masy.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI inayojihusisha na utoaji wa huduma za matangazo ya luninga kwa njia ya dijitali, StarTimes Tanzania imepokea ugeni mzito wa aliyekuwa mchezaji nguli wa kikosi cha Nigeria au Super Eagles na Arsenal ya Uingereza, Bw. Nwankwo Kanu ambaye kwa sasa ni balozi wa kampuni hiyo kwa bara la Afrika ambamo imo kwenye takribani nchi zaidi ya 10.



Akizungumza mara baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jana usiku, mchezaji Nwankwo Kanu alisema kuwa anajisikia furaha kubwa kuwasili Tanzania salama kujumuika na kmapuni ya StarTimes katika shughuli mbalimbali kwa ndani ya kipindi cha siku tano atakazokuwepo.



‘’StarTimes ni kampuni kubwa barani Afrika na imeleta mapinduzi makubwa katika upande wa matangazo ya luninga kwa dijitali kwani imeweza kutoa huduma zake kwa ubora mkubwa na gharama nafuu ambazo kila mtu anaweza kuzimudu.’’



Kwa upande wa vipindi na chaneli za michezo mchezaji Kanu amebainisha kuwa kampuni ya StarTimes imepiga hatua kubwa hasa kwa upande wa kupata na kuonyesha michezo ya ligi ya soka kubwa barani Ulaya kama vile za Bundesliga na Serie A za Ujerumani na Italia.



“Mimi kama balozi wa StarTimes barani Afrika nitajitahidi kawa kadiri ya uwezo wangu kuwa kiungo muhimu katika kuhakikisha ninaiwakilisha vema kwa wateja wake, hususani katika shughuli mbalimbali kama vile soka kama mjuavyo ni mchezo unaopendwa na watu wengi duniani na hata miongoni mwa waafrika wenyewe.” Aliongezea Kanu.



“Hivyo basi kwa muda wote nitakaokuwepo nchini Tanzania nitashirikiana na StarTimes kwa ukaribu katika shughuli za kikampuni na pia za kijamii kama vile za kielimu na afya. Kama mjuavyo katika mahala popote unapofanyia shughuli zako ni muhimu sana kuijali jamii inayokuzunguka kwani yenyewe ndiyo sababu kubwa ya wewe kuwepo.” Alihitimisha



Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes nchini, Bw. Lanfang Liao amesema kuwa, “Uwepo wa Kanu Tanzania ni fursa ya kipekee na pia ni moja ya jitihada kubwa za kampuni yake katika kuimarisha na kuhudumia wateja wao hususani kwa vipindi vya michezo na burudani na ninaamini uwepo wake utaleta chachu kwetu sisi na wateja kwa ujumla.”



“Nwankwo Kanu alikuwa ni mchezaji wa kimataifa si tu aliiwakilisha nchi yake ya Nigeria kimatifa katika michuano mbalimbali lakini pia alifungua milango kwa vipaji vya Afrika barani Ulaya. Hivyo basi tunaamini bado ni maarufu na ana heshima kubwa miongoni mwa watanzania na wapenda soka barani Afrika. Kwa yeye kuwa balozi wetu ninaamini tutafaidika kwa namna gani tuboreshe huduma zetu ili kuiteka mioyo ya watanzania na waafrika kiujumla.” Alimalizia Bw. Liao

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.