Habari za Punde

Timu ya Kivumbi Yaendelea Kutoa Takrima kwa Wapinduzi I

Na.Mwandishi Wetu.

Timu ya soka ya Arfican Kivumbi kutoka Mwambe kisiwani Pemba imeendelea kutoa alama tatu muhimu kwa wapinzani wake kufuatia kichapo cha bao 2-0 walichopata leo hii.


Timu hiyo iliyoshuka dimbani FFU, Finya jioni ya leo hii imepata kipigo hicho kutoka kwa timu kongwe kutoka wilaya ya Chake chake, timu ya Chipukizi.Pambano hilo ambalo ni muendelezo wa ligi kuu ya soka zanzibar hatua ya nane bora ulianza kwa timu hizo kushambuliana kwa zamu na kulipeleka pambano hilo mapumziko pasipo kufungana.Kipindi cha pili Chipukizi walionyesha uchu zaidi wa kutafuta ushindi na kufanikiwa kupata mabao hayo mawili kupitia mshambuliaji wao Mussa Ali.Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa michezo miwili kule Pemba, Jamhuri watachuana na mahasimu wao wakubwa kutoka jiji la Wete timu ya Mwenge.Uwanja wa Amaan mjini Unguja, Zimamoto watatoana jasho na maafande wenzao wa JKU.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.