Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli Azuru Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume wakati wa Ziara Yake Zanzibar.


 
Jengo la Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar. 
Mke wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Mama Fatma Karume akisalimiana na Katibu wa Mufti wa Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Fadhil Soraga alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM kuhudhuria ziara ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli, kutembelea kaburi la Marehemu Karume kwa kusoma dua.  
Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akisalimiana na Naobi Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai alipowasili katika Afisi Kuu ya CCM kuhudhuria ziara ya Rais Dk Magufuli kuzuru kaburi la Marehemu Mzee Abeid Karume. kisiwandui Zanzibar. kushoto Meya wa Mji wa Zanzibar Mstahiki Meya Khatib Abdurahaman.  
Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akisalimiana na Mama yake Mama Fatma Karume baada ya kuwasili katika viwanja hivyo vya Afisi Kuu kuhudhuria ziara ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kudhuru kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
Waheshima  Wakuu wa Wilaya wakizungumza na Meya ya Manispa ya Zanzibar Mhe Khatib Abdurahaman Khatib wakati wakimsubiri Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika ziara yake kutembelea Zanzibar na kuzuru kaburi la Marehemu Mzee Aneid Amani Karume Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud Mohammed akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Anayeshughulikia Muungano Mhe Januari Makamba wakiwa katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar. 
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Balozi Ali Karume akizungumza na Mawaziri wa SMZ na SMT wakati wakimsubiri Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kuzuru kaburi la Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume. kutoka kushoto Mhe Januari Makamba, Mhe Haji Omar Kheri na Mhe Issa Haji Gavu wakiwa makini wakimsikiliza Balozi Ali Karume. 
Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk Amani Karume, Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Mama Fatma Karume na Balozi Ali Karume wakiwa na Viongozi wa Serikali na Chama wakijiandaa kumpokea Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kuaza ziara yake kuzuru kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.   
Viongozi wa Serikali na Chama wakiwa katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
Watoto wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume, wakiwa katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kumpokea Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli, wakiwa na Mama yao Mama Fatma Karume, Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume na Balozi Ali Abeid Karume.  
Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Dk John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar kuaza ziara yake kwa kuzuru kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.akipokelewa kwa bwaride maalum la Jeshi la Wananchi wa Tanzania lililoandaliwa kwa ajili yake. 
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume baada ya kuwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar kuaza ziara yake kwa kuzuru kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume. 
Rais wa Jamuhri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli akisalimiana na Mtoto wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, Balozi Ali Abeid Karume. 
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli, akisalimiana na Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Mama Fatma Karume alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar kuaza ziara yake kwa kudhuru kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume. 
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli akisalimiana na Mstahiki Meya wa Mji wa Zanzibar Mhe Khatib Abdurahaman Khatib.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Hamad Masauni alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kuzuru kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
Rais wa Jamuhguri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli akisalimiana na Mhe Haroun Ali Suleiman. 
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli akielekea katika eneo la kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume kumuombea dua wakati wa ziara yake ya siku mbili Zanzibar kuzungumza na Wananchi wa Zanzibar na kutowa shukrani kwa kumchagua kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.katika uchaguzi Mkuu wa mwaka jana 2015.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli akiwa katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume alipofika kuzuru kaburi hilo la kumuombea dua wakati wa ziara yake ya Siku mbili Zanzibar.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli akiweka Shada la Maua katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume wakati wa ziara yake Zanzibar kwa kuaza kuzuru kaburi hilo lilioko katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli akiomba dua baada ya kuweka Shada la Maua katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume kisiwandui Zanzibar.
  
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.