Habari za Punde

Waziri wa Fedha ziarani Pemba kukagua miradi


MKANDARASI kutoka ya Mekon Consultant Engineering ya Tanzania bara, Joseph Maradu ambayo kampuni hiyo ndio inayolifanyia matengenezo makubwa, ofisi ya Baraza la mji Mkoani, akimpa maelezo ya matengenezo hayo Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe: Khalid Salum Mohamed, wakati alipofika hapo kuangalia maendeleo ya matengenezo hayo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe: Khalid Salum Mohamed, akizungumza mara baada ya kukagua matengenezo ya ofisi ya baraza la mji Mkoani Pemba, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tatu kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe: Khalid Salum Mohamed akiangalia karafuu kwenye kituo cha kununulia cha ZSTC Mkoani, wakati alipofika hapo kuangalia zoezi hilo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

MDHAMINI wa Shirika la taifa ZSTC Pemba, Abdalla Ali Ussi, akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe: Khalid Salum Mohamed, wakikagua karafuu ambazo zimeshanunuliwa na ZSTC kituo cha Mkoani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe: Khalid Salum Mohamed, akizungumza na wakulima za wazo la karafuu waliofika kituo cha ZSTC Mkoan kuuza karafuu zao, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe: Khalid Salum Mohamed akikagua karafuu ambazo tayari kawa ajili ya kusafirishwa Unguja ambazo zimeshanunuliwa na ZSTC Mkoani wakati waziri huyo alipofika kituoni hapo kuangalia zoezi la ununuzi wa karafuu hizo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.