Habari za Punde

Uzinduzi wa Kitabu cha Muongozo wa Mabaraza ya Watoto Zanzibar.



Ofisa Mdhamini Wizara ya Fedha Pemba, Ibrahim Saleh Juma, akitowa neno kabla ya kukizinduwa kitabu cha mwongozo wa Mabaraza ya watoto Zanzibar, huko katika ukumbi wa kiwanda cha mafuta ya makonyo Wawi Pemba.
 Ofisa Mdhamini Wizara ya Fedha na Mipango -Pemba, Ibrahim Saleh Juma, akizinduwa Kitabu cha Mwongozo wa Mabaraza ya Watoto Zanzibar huko katika ukumbi wa mafuta ya makonyo Wawi-Pemba.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mabaraza ya watoto Zanzibar, Mundhir Hamran Said, akiinuwa Kitabu pamoja na Ofisa kuto Save the Children , huko katika ukumbi wa makonyo wawi mara baada ya kuzinduliwa rasmi na Ofisa mdhamini Wizara ya Fedha Pemba.
 Baadhi ya watoto kutoka katika maeneo mbali mbali ya Kisiwa cha Pemba, wakimsikiliza Ofisa mdhamini Wizara ya Fedha na Mipango-Pemba, Ibrahimu Saleh Juma, akitowa nasaha zake kwa watoto juu ya kitabu cha  Muongozo wa mabaraza ya Watoto Zanzibar.
 Baadhi ya watoto kutoka katika maeneo mbali mbali ya Kisiwa cha Pemba, wakimsikiliza Ofisa mdhamini Wizara ya Fedha na Mipango-Pemba, Ibrahimu Saleh Juma, akitowa nasaha zake kwa watoto juu ya kitabu cha  Muongozo wa mabaraza ya Watoto Zanzibar.
 Wadau kutoka Save the Children, wakifuatilia kwa makini uzinduzi wakitabu cha mwongozo wa mabaraza ya watoto Zanzibar , uliofanyika katika ukumbi wa kiwanda cha mafuta ya makonyo Wawi Pemba.(Picha na Bakar Mussa Pemba.)

Na Salmin Juma, Pemba

Jamii imetakiwa kuacha tabia zinazoweza kuwanyima watoto haki zao za msingi na badala yake wawajengee  ustawi mzuri wa maisha  ya baadae.

Afisa mdhamini wizara ya fedha na uchumi Pemba Ibrahim Saleh Juma ameyasema hayo huko ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Pemba alipokuwa akizindua kitabu cha muongozo wa mabaraza ya watoto chenye lengo la kuimarisha haki na wajibu katika kutoa maamuzi juu ya mambo yanayohusu.

Amesema kuna baadhi ya wazazi na walezi huwavunjia haki watoto kwa kuwaozesha na kuwakosesha elimu ya msingi jambo ambalo huleta migogoro miongoni mwa jamii.

Katika risala yao watoto hao wameiomba Serikali na viongozi wengine kuyapa kipaumbele masuala ya watoto kwa kuimarishwa ulinzi utakaosaidia kuondoa vitendo vya unyanyasaji kwa watoto hao .

Wamesema  mabaraza yamekuwa yakikabiliwa na changamoto nyingi hivyo ni budi kwa serikali kuwategea bajeti itakayoweza kuboresha hali ya mabaraza hayo ili lengo la uzinduzi wa kitabu hicho liweze kufanikiwa.

Akielezea lengo la kitabu hicho mwekiti wa badi ya ushauri ya  baraza la watoto Zanzibar Mundhir Hamad Said amesema kupitia muongozo huo watoto watapata fursa ya kuachwa huru kutoka katika mazingira  hatarishi na vitendo vya udhalilishaji kutoka kwa jamii .


Uzinduzi huo wa kitabu cha muongozo wa mabaraza ya vijana Zanzibar umefadhiliwa na shirika na huwahifadhi watoto ulimwenguni la Save the children kikiwa na kauli mbiu ya kulindwa , kushirikishwa ,kupata hifadhi ,chakula, afya bora na kuelimishwa .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.