Habari za Punde

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanawema Shein, Azungumza na Viongozi wa Madhehebu ya Dini ya Kikristo na Kuzindua Albam ya Kikundi cha Kwaya cha Kanisa la R.G.C Chakechake

 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Viongozi wa Madhehebu ya Dini ya Kikristo, wakati akiwasili katika ukumbi wa Chuo cha Amali Vitongoji kuzungumza na Waumini hao na kuwazindulia Albam yao iliokuwa na Ujumbe wa Kudumisha Amani Zanzibar ijulikasnoyo kwa jina Mungu Baba.ikiwa na nyimbo kumi na moja za kuitakia Amani Zanzinar na Tanzania.  
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiangalia bidhaa za Wajasiriamani wa Kikundi cha Nia Njema Wete kinachojishughulisha na utengenezaji wa Vipochi na mikoba.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiangalia bidhaa za Wajasiriamani wa Kikundi cha Nia Njema Wete kinachojishughulisha na utengenezaji wa Vipochi na mikoba.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman wakiingia katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Amali Vitongoji Chake kwa ajili ya kuzungumza na Waumini wa Madhehebu ya Dini ya Kikristo na kutowa shukrani kwa ushirikiano wao na kuwazindua  Albam ya Kikundi cha Kwaya cha Kanisa la R.G.C la Chakechake Pemba.
Viongozi wa Madhuhebu ya Dini mbalimbali wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakati Mke wa Rais wa Zanzibar akiingia katika ukumbi huo wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji .
Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Pemba Mhe Salama Mbarouk akizungumza wakati wa mkutano huo wa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, na Waumini wa Madhehebu ya Dini ya Kikristo kisiwani Pemba katika Ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji.
Kaimu Naibu Katibu wa UWT Zanzibar Tunu Kondo akizungumza machache kabla ya kuaza kwa mkutano huo na Viongozi wa Dini ya Kikristo kisiwani Pemba kutowa nasaha zake na kuwashukuru kwa ushirikiano wao katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Waziri wa Vijana Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Moudline Castico akizungumza wakati wa mkutano huo na viongozi wa Dini kisiwani Pemba katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji.  
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman akitowa nasaha zake kwa waumini hao wajkati wa mkutano huo wa kutowa shukrani na kuzinduliwa albam yao ya kwaya ya kanisa la RGC Chakechake, ikiwa na nyimbo za kulitakia Taifa Amani. iliozinduliwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.
Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume akitowa nasaha zake na kutowa historia ya Zanzibar kwa waumini hao wakati wa mkutano wa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Amali Vitongoji Pemba. 
Waumini wa Dini wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakifuatilia nasaha zinazotolewa.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia Waumini wa Dini mbalimbali za Kikristo kisiwani Pemba akiwa katika ziara yake kutowa shukrani kwa Viongozi wa UWT na Wananchi kwa kushiriki vizuri katika uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliopita na kukipatia Chama ushindi. 
Mke wa Rais wa Zanzibar akiwahutubia na kutowa nasaha zake kwa Waumini wa Dini wakati wa mkutano wake huo wa kuwashukuru na kuzinduia Albamu ya Kikundi cha Kwaya ya Kanisa la RGC Chakechake iliobeba nyimbo 11 zikiwa na Ujumbe wa Kulitakia Taifa la Zanzibar na Tanzania Amani, mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji Pemba.  
Viongozi wa Dini wakifuatilia hutuba ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakati akizungumza na viongozi hao na baadhi wa waumini wao katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha mafunzo ya amali vitongoji Pemba.
Waumini na Viongozi wa Dini wakiwa katika ukumbi wa mnkutano wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia wakati wa hafla hiyo.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akikabidhiwa Albam ya Nyimbo Mpya za Kwaya za Kanisa la RGC Chakechake kwa ajili ya kuizindua Albam hiyo ikiwa na nyimbo 11 za kulitakia Taifa Amani na Utulivu kwa Wananchi wake. akikabidhi Albam hiyo Kiongozi wa Kwanya hiyo Happnoah Mwanana. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizindua Albam Mpya ya Kwaya ya Kanisa la RGC Chakechake Pemba kulia Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman na Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Zanzibar Emmanuel Masoud, wakishuhudia uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha amali vitongoji Pemba. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akionesha Albam hiyo baada ya kuizindua rasmin katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji Pemba.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman na Mama Fatma Karume wakiangali gamba la Cd hiyo ya Nyimbo za Kwaya ya Kanisa la RGC, baada ya kuzinduliwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein. 
Kikundi cha Kwaya ya RGC Chakechake wakiimba moja ya wimbo ilioko katika Albam hiyo ya Mungu Baba iliozinduliwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein. wakiwa katika ukumbi huo. 
Waziri Moudline Castico ameshindwa kujizuiwa wakati wa uzinduzi huo ikiimbwa moja ya nyimbo zilizokuwemo katika albam hiyo na kutokwa na machozi.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizindua harambee ya kuchangia kwaya hiyo wakati wa uzinduzi huo na kutowa shukrani zake kwa Waumini hao kwa ushirikiano wao kwa Mama Mwanamwema Shein, katika harakati zake za kuleta maendeleo kwa Jamii Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.