Habari za Punde

Shumba Viamboni kufaidika na maji safi na salama

Na Salmin Juma, Pemba

Zaidi ya watu elfu tatu wa vijiji nane vya shehia ya Shumba Viamboni Wilaya ya Micheweni wanatarajiwa kufaidika na huduma ya maji safi na salama baada ya kukamilika kwa kazi ya uwekaji wa mabomba ya kusambazia maji kutoka katika kisima kipya kilichochimbwa katika shehia hiyo.

Afisa mdhamini wizara ya maji ,ujenzi, nishati na ardhi, Juma Bakar Alawi amewataka wananchi hao kushirikiana katika kukamilisha ufungaji wa mabomba hayo ili kuona kwamba kila mmoja anafaidika na maji hayo.

Naye Sheha wa Shehia ya Shumba Viamboni, Time Said Omar amesema huduma hiyo ya maji safi na salama itatoa mchango mkubwa wa kimaendeleo hasa kwaakinamama kutokana na kuwa wengi wao walikuwa wakiifuata amasafa yambali na kukosa kushiriki katika kazi zao za kijamii.

Wakizungumza baadhi ya wananchi wa Shehiya hiyo wamesema mbalina kuishukuru Serikali katika upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama bali itarahisisha kuwepo kwa ukaribu na familia zao nakuepusha upatikanaji wamaradhi ya kuambukiza na matumbo ya kuharisha .

Vijiji ambavyo vimelengwa kunufaika na huduma hiyo ni pamoja na Kichungwani, Muondoni, Gombe, Nguuni, Mikinduni, Uondwe na Uwaani .

Kisima hicho cha maji safi na salama cha Shumba Viamboni ambacho kimechimbwa na kwa nguvu za wananchi na Serikali kinakadiriwa kuwa hudumia na wananchi wa ndani na walionje na shehia hiyo ikiwemo Bule na baadhi ya vijiji vya Tumbe

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.