Habari za Punde

Ufunguzi wa Majengo Mapya ya Wodi ya Kinamama na Watoto Katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar na Rais wa Zanzibar Dk Shein.

Jengo Jipya la Wodi ya Watoto katika hospitali ya Mnazi Mmoja lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar Dk Shein. 

Jengo Jipya la Wodi ya Wazazi katika hospitali ya Mnazi Mmoja lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar Dk Shein.  
Viongozi wa Serikali na Wawakilishi wa Balozi wakiwa katika viwanja vya Majengo Mepya tya Wodi za Wazazi na Watoto katika hospitali ya Mnazi Mmoja wakimsubiri kumpokea mgeni Rasmin Rais wa Zanzibar Dk Shein, kwa ajili ya kuyafungua majengo hayo.
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Muwakilishi wa Ubalozi wa Norway Tanzania Meneja Miradi ya Ubalozi Tanzania Victor Mlunde, alipowasili katika viwanja majengo hayo kwa ajili ya uzinduzi wake.
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland Norway Bwa, Eivind Hansen, alipowasili katika viwanja majengo hayo kwa ajili ya uzinduzi wake. 
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Muwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Tanzania, Bi Theresia Mcha,alipowasili katika viwanja majengo hayo kwa ajili ya uzinduzi wake. 
Rais wa Zanzibar na Mqwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo alipowasili katika viwanja vya majengo Mapya ya Wodi za Watoto na Kinamama katika viwanja vya hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kwa ajili ya uzinduzi wa majengo hayo mawili.   
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Muwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Tanzania Bi Theresia Mcha, akikata utepe kuashiria kufungua jengo la Wodi ya Wazazi Zanzibar katika eneo la Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Muwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Tanzania Bi Theresia Mcha na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakishangilia baada ya Uzinduzi wa Wodi hiyo ya Wazazi Zanzibar. ikiwa ya Kisasa.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Tanzania Bi Theresia Mcha wakiwa katika jengo hilo baada ya kulifungua rasmin kulia Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.wakitembelea jengo hilo baada ya uzinduzi wake. 
Mkandarasi wa Majengo ya Wodi ya Wazazi na Watoto wa Kampuni ya Ujenzi  Rans Ndg. Ali Nassor Salim. akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, michoro ya jengo hilo baada ya ufunguzi wake, kulia Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, na kushoto Mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Tanzania Bi Theresia Mcha.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akitembelea Wodi ya Wazazi baada ya kulizindua Jengo hilo, lilioko katika eneo la Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.   
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mtaalamu wa Mashine ya X-Ray katika hWodi ya Wazazi Ndg Jaykishan Murj wakati akitembelea katika wodi hiyo kujionea vifaa mbalimbali vya kisasa vilioko katika jengo hilo kwa ajili ya kutowa huduma kwa Wazazi wanaofika kujifungua katika Hospitali hiyo Mpya ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Wageni waalikwa kutoka Norway na Uholanzi wakihudhulia katika ufunguzi huo wa Wodi za Watoto na Wazazi Hospitali ya Mnazi Mmoja Zabnzibar. 
Mtaalamu wa Umeme wa nguvu za jua akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, wakati akitembelea Jengo hilo la Wazazi na kutembelea chumba maalum cha mitambu ya umeme wa jua wakati umeme wa kawaida utakapokatika na kutumika umeme huo wa jua katika majengo hayo ya hospitali ya Wazazi na Watoto Mnazi Mmoja. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein. akiwa katika chumba maalum cha umeme wa Solar katika majengo hayo, wakati akipata maelezo kutoka kwa wataalam.   
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akimsikiliza Muunguzi wa Wodi ya Wazazi akitoa maelezo ya moja ya mashine za kisasa katika jengo hilo zitakazotumika kutowa huduma kwa Wamama Wajawazito katika Wodi hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiondosha kipazia kuashiria kulifungua Jengo la Wodi ya Watoto katika viwanja vya hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kulia Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo, Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya  Chuo Kikuu cha Haukeland Norway Bwa. Eivind Hansen na Mwakilishi wa Ubalozi wa Norway Tanzania Meneja Miradi ya Ubalozi Tanzania Ndg Victor Mlunde.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, na Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland Norway Bwa. Eivind Hansen. wakikata utepe kuashiria kulizindua jengo la Wodi ya Watoto katika eneo la hospitali ya Mnazi Mmoja litakalotoa huduma kwa Watoto na Wazazi katika hospitali hiyo Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo wakielekea sehemu maalumu ilioandaliwa baada ya ufunguzi wa Majengo ya Hospitali ya Wazazi na Watoto iliojengwa katika eneo la Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.