Habari za Punde

Taarifa ya Michezo ya Kombe la Mapinduzi 2017. Zanzibar


Kamati ya kusimamia mashindano ya Kombe la Mapinduzi (Mapinduzi Cup) imo katika matayarisho ya michuano hiyo baada ya kuzinduliwa rasmi na Katibu Mkuu Wizaraya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo.

Mashindano ya Mapinduzi Cup yatakayoshirikisha timu tisa kutoka Uganda, Tanzania Bara na wenyeji Zanzibar yatafanyika katika uwanja wa Amani kuanzia  tarehe 30 mwezi huu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi ni Sharifa Khamis na Katibu wa Kamati hiyo ni Khamis Abdalla Said.

Wajumbe wa Kamati ni Ali Khalil Mirza, Khamis Mzee Ali, Juma Mmanga, Ravia Idarous Faina, Mohammed Ali, Mohammed Ali Hilal, Issa Mlingoti Ali, Dk. Ally Saleh Mwinyikai na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Omar Hassan Omar ‘King’.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.