Habari za Punde

Udhalilishaji Bado ni Tatizo Pemba.

 Askari ya Jesho la Polisi wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Kupinga Udhalilishaji wa Kijinsia yalioadhimisha Wilaya ya Wette Pemba na kuhuubiwa na Naibu wa Wizara ya Afya Zanzibar Mhe. Harusi Said Suleiman.
Wananchi wakiwa na mabango ya kupiga vita udhalilishaji wa Kijinsi wakati wa sherehe za maadhimisho yake yaliofanyika Kisiwani Pemba Wilaya ya Wete.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar Mhe, Harusi Said Suleiman akitowa nasaha zake kwa Wananchi wa Kisiwani Pemba wakati wa maadhimishi ya Siku hya Udhhalilishaji Kijinsia na kuwataka wananchi kupiga vita vitendo hivyo kwa nguvu zao zote. 


Na mwandishi wetu.
Jeshi la polisi limetakiwa kutozifumbia macho kesi za ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ambazo zimeonekana kushamiri siku hadi siku.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri Wizara ya Afya Zanzibar Mh. Harusi Saidi Suleiman katika maadhimisho ya 16 za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto  yaliofanyika katika Viwanja vya Jamhuri Wete kusini Pemba.

Amesema  jamiii  inashindwa kupeleka kesi hizo mahakani  kutoka na kucheleweshwa kwa baadhi ya kesi na kuchukua muda mrefu jamba ambalo linavunja moyo kwa waliopata matatizo kama hayo .

Amefahamisha kua kutokana na Polisi kuzichelewesha kesi hizo ndio imepelekea jamii  kuzisuluhisha wenyewe kwa wenyewe  na ndio sababu ya ongezeko  la matendo ya ukatili wa  kijinsia. 

Ameliomba jeshi la Polisi na jamii kwa ujumla  kushirikiana kwa pamoja ili kutokomeza vitendo hivyo ambavyo kwa sasa vimeonekana kushika kwasi wa vijana hasa wa kiume.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman kupitia maadhimisho hayo amepiga marufuku uoneshwaji wa luninga maeneo ya nje akidai kua kitendo hicho kimechangia kwa asilimia kubwa vijana na watoto kujiingiza katika vitendo viovu.

Pia amelitaka  jeshi la polisi kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakao bainika kuonyesha televisheni nje na adhabu kali zitolewe juu yao kwa kupinga amri hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa Wa Kaskazini Pemba Haji Khamis Haji amesema kuundwa kwa madawati ya kupinga ukatili wa kijinsia kunaweza kupunguza vitendo hivyo lakini ni pale  jamii itakapo ushirikiano wake

Awali akisoma risala katika maadhimisho hayo  Mwakilishi wa Jeshi la Polishi kutoka mtandao wa Polisi wanawake mkoa wa Kaskazini Pemba amesema ukosefu  wa kipimo cha DNA na ofisi za madawati ni miongomi mwa changamoto zinazo wakabili katika utendaji wao wakazi.

Amesema ucheleweshwaji wa kutolewa maamuzi kwa  kesi zianazopelekwa mahakamani  kuna sababisha baadhi ya watu kukata tama mapema  juu ya kesi zao  na mwisho kukosa mashahidi waliojitolea kutoa ushahidi juu ya vitendo husika.

Amesema jamii imekosa ujasiri juu ya kuwakamata wahalifu wanaofanya matendo hayo ikiwemo unyanyasaji mkubwa wa liwati ambao umeshika kasi kwa jamii.

Aidha amesema kuwa  jumla  ya  kesi 74 zimeripotiwa kwa mwaka 2016 ambapo kesi 16 mashauri yake yanaskilizwa kesi 24 zimetolewa hukumu kwa watuhumiwa kutumikia kifungo, kesi 3 zipo kwa mkemia mkuu wa serekali na kesi 26 zinaendelea na upelelezi.

Ujumbe wa mwaka huu katika maadhimisho hayo ni Funguka Pinga Ukatili wa Kijinsia Toa Elimu Salama Kwa Wote.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.