Habari za Punde

Wananchi watakiwa kuzitathmini skuli zao za karibu

Na Salmin Juma, Pemba

Wananchi wa wilaya ya Chakechake kisiwani Pemba wametakiwa kuzijali na kuzithamini skuli za karibu yao badala ya kukimbilia kuwapeleka  watoto wao skuli za mbali  na zinazotoza ada kubwa za kusomeshea na gharama nyenginezo wakati skuli za karibu zipo na ubora wake ni sawa au umepindukia huko.

Hayo yamesemwa leo na mgeni rasmi wa katika  ya sherehe ya kuwaaga wanafunzi wa darasa la sita  wa skuli  ya Akhalil English Medium school iliyopo Mtoni chakechake Pemba  sheikh Zahor Saleh Omar ambae ni katibu mkuu wa Zanzibar Children Fund (ZCF) na mkurugenzi wa skuli hiyo.

Kwa kulithibitisha hilo Sheikh Zahor amesema skuli hiyo imeshika nafasi ya tatu katika ya skuli zisizopungua ishirini na tano kiwilaya na kusema kua hiyo ni dalili tosha ya kuonesha  kua skuli ya Alkhalil ni bora na inayohitaji kuungwa mkono na wazazi na jamii kwa ujumla kwa kuwapeleka watoto katika skuli hiyo.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi mwenyekiti wa kamati ya wazazi wa skuli ya Alkhalil Hafidh Mbarouk amesema wazazi na walezi wa watoto hakuna budi jumuku la malezi kulibeba kwa pmoja ili kujua maendeleo ya mtoto, ambapo amesema kua katika hali ya kawaida watoto muda mwingi huwa katika mikono ya wali, hivyo wazazi kujiona kua ndio wameshamaliza kazi

“Kuanzia asubuhi mtoto wako anakua skuli na akirudi anapumzika muda mfupi tu kisha anakwenda madrasa sasa muda mwingi anakua mikononi mwa mwalimu, hivyo wazee musiitumie fursa hiyo kama ndio mumeshamaliza kazi badala yake pia mutoe mashirikiano ya dhati kwa walimu kufanikisha ulezi wa watoto”alisema Mbarouk.

Haya ni mahafali ya nane kufanyika, Skuli ya Alkhalil inafundisha watoto katika ngazi ya Nursery hadi darasa la sita, inawalimubora wenye uzoefu wa hali ya juu. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.