Habari za Punde

Mchezo wa Simba na Taifa ya Jangombe Kombe la Mapinduzi Cup Usiku.

 Wapenzi wa mchezo wa Soka Zanzibar wakiwa katika jukwaa la urusi wakifuatilia mchezo huo wa kombe la Mapinduzi Kati ya Simba na Taifa ya Jangombe Wakombozi wa Ng'ambu.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Jangombe wakiwasili katika Uwanja wa Amaan Zanzibar Tayari kuanza kwa mchezo wao wa pili wa Kombe la Mapinduzi baada ya mchezo wao wa kwanza wa ufunguzi kutoka kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Timu ya Jangombe Boys mchezo uliofanyika wiki iliopita.

Mbunge wa Jimbo la Jangombe Mhe Mr. White akielekea katika vymba vya wachezaji wa timu yake ya Taifa ya Jangombe.
Wachezaji wa Timu ya Simba wakiwasili katika uwanja wa Amaan kuaza mchezo wao wa kwanza na Timu ya Taifa ya Jangombe.


Waamuzi wa mchezo wa Simba na Taifa ya Jangombe wakipasha misuli kabla ya kuanza kwa mchezo huo wa Kombe la Mapinduzi Cup Zanzibar.
Wachezaji wa Timu ya Simba wakipasha kabla ya kuanza kwa mchezo huo wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa Amaan.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.