Habari za Punde

Mgombea Ubunge Kupitia CCM Ali Juma Ali Katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Dimani Aibuka Kidedea kwa Ushindi wa Kura Nyingi.

Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Dimani Zanzibar  kupitia Chama cha Mapinduzi Ndg Ali Juma Ali ameibuka mshinda katika uchaguzi huo uliofanyika jamapili 22-1-2017 kwa ushindi wa Kura 4,860, kuwa mshindi katika uchaguzi huo Mdogo wa Jimbo la Dimani kufuatia kwa Kifo cha Aliyekuwea Mbunge wa Jimbio hilo Marehemu Hafidh Ali Tahir, kilichotokea mwezi wa Novemba 2016.

Jumla ya Vyama vya Siasa 11 vimeshiriki katika Uchaguzi huo mdogo wa Jimbo la Dimani Zanzibar idadi ya Wananchi waliojiandikisha katika daftari la Wapiga Kura 9,275 na idadi halisi ya Wananchi waliojitokeza kupiga Kura katika uchaguzi Mdogo wa Jimbo hilo ni 6,406, Idadi ya Kura halisi ni 6,172.

Mgombea wa Chama cha Mapinduzi ameshinda katika uchaguzi huo kwa ushindi wa kura halali 4,860, na kutangazwa mshindi na Afisa wa Uchaguzi wa Tume ya Uchaguzi Wilaya ya Magharibi Unguja Bi Fatma Gharib, mshindi wa Pili ni Mgombea wa Chama cha CUF Ndg. Abrazaka Khatib kwa kupata Kura 1,234. na Vyama vyengine vimepata kura kama ifuatovya. Chama cha  ACT  kura 8, ADC 42, CHAUMA 10, DP 8, NRA 1,SAU 4,TLP 2, UMD 2 na UPDP kura 1.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.