Habari za Punde

Waziri wa Fedha afungua Jengo la Baraza la Mji wa Mkoani - Pemba katika shamrashamra za miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar

 Mhandisi mkuu wa Kampuni ya Ujenzi wa ZEECON, akitowa maelezo ya ujenzi huo wa Ofisi ya Baraza la Mji mkoani-Pemba.
 Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt, Khalid Salum Ali, akikata Utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Baraza la Mji wa Mkoni ikiwa ni shamra shamra ya miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar.

 Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Mkoani Pemba, kabla ya kumkaribisha Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt, Khalid Salum Muhammed, katika ufunguzi wa Jengo la Baraza la Mji wa Mkoani-Pemba, ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar.
 Mhandisi wa Kampuni ya Zeecon, akitowa maelezo juu ya ujenzi huo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Khalid Salum Ali  na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdalla, huko katika jengo la Baraza la Mji Mkoani Pemba.
Jengo la Baraza la Mji Mkoani Pemba, ambalo lilifanyiwa matengenezo makubwa, ambalo limefunguliwa na Waziri wa fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar.

Picha na Habiba Zarali -Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.