Habari za Punde

Mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Dr. Abdallah Juma Mabodi Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk Abdallah Juma Mabodi, akiwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar baada ya kuteuliwa wiki iliopita kuchukua Nafasi ya Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai, mapokezi hayo yamefanyika katika viwanja hivyo leo asubuhi akitoea Jijini Dar es Salaam.   Kulia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Ndg Borafia Naibu Katibu Mkuu CCM Mstaaf Ndg. Vuai Ali na Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani Mhe Ali Salum na kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhani.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdallah Juma Mabodi akivishwa kiskafu na Kijana wa Chipukizi baada ya kuwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar akisalimiana na Viongozi na Wanachama wa CCM waliofika kumpokea katika viwanja vya CCM Zanzibar.



Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdallah Juma Mabodi akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Welezo Mhe. Hassan Diaspora alipowasili katika viwanja vya CCM Zanzibar. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr Abdallah Juma Mabodi akiwa na furaha akisalimiana na Ndg Kimara katika viwanja vya CCM Zanzibar. 

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdallah Mabodi akiwa na Naibu Katibu Mkuu Mstaaf Ndg Vuai Ali Vuai wakielekea katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume kuomba dua ikiwa ni shamrashamra za mapokezi yake.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr Abdallah Juma Mabodi akiwa na Viongozi wa CCM na Wananchi wakiitikia dua iliokuwa ikiombwa katika kaburi la Marehemu Mzee Abeid Amani Karume Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Muasisi wa Afro Shirazi ASP.









No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.