Habari za Punde

Ujenzi wa barabara ya Madanjani Mzambarauni Takao wafikia hatua ya uwekaji lami

Na Mwandishi wetu

Wizara ya ujenzi mawasiliano na usafirishaji Pemba imesema matengenezo ya barabara ya Madanjani Mzambarauni Takao yamekamilika kwa asilimia 80% na tayari mafundi wa ujenzi wakiwa katika hatua uwekaji wa lami ya maji.

Afisa Mdhamini wa Wizara ya ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Pemba Hamad Ahmed Baucha amesema matengenezo ya ujenzi huo yamefikia hatua ya kuweka lami ya maji na mafundi wako katika hatua ya mwisho ya kuweka kifusi ili kukamilisha ujenzi huo 

Baucha amesema barabara hiyo ya kilomita tano  ambayo itakuwa na vituo vitano vya kushusha na kupandia abiria  inatarajiwa kukamilika kabla ya wakati baada ya mkandarasi kuelezea kuelezea hayo .

Meneja wa ujenzi wa barabara ya Madenjani Mzambarauni Takao Juma Othman Mussa amesema kwamba itakuwa na ubora zaidi ya barabara iliyokuwepo ambayo maeneo mengi yalikuwa yameshakatika

Nao baadhi ya wananchi waliozungumza kuhusiana na maendeleo ya matengenezo hayo wamesema kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo utawasaidia kuendeleza shughuli zao mbalimbali za kiuchumi kuliko hapo awali.

Matengenezo ya ujenzi wa barabara ya Madenjani  Mzambarau Takao unaofadhiliwa na mfuko wa barabara na yanayofanywa na Kampuni ya Mecco yatagharimu zaidi shilingi bilioni moja ya Kitanzania

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.