Habari za Punde

Wafanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar(PBZ) Tawi la Forodhani Unguja Wamuaga Meneja wao Said Mwinyogogo na Kumkaribisha Meneja Mpya Mohammed Nuhu.

Wafanyakazi wa Tawi la Benki ya Watu wa Zanzibar Forodhani wakiwa katika picha ya pamoja wakimuaga na kumkabidhi keki wakati wa hafla ya tafrija ilioandaliwa na Wafanyakazi hao kwa bosi wao katika ukumbi wa Hoteli ya Park Forodhani Zanzibar.
 Afisa wa Benki ya Watu wa Zanzibar Tawi la Forodhani Unguja Rashida Mohammed akimkabidhi Keki wakati wa hafla hiyo ya kumuaga waliomuandalia katika ukumbi wa hoteli ya Park Forodhani Unguja anayeshuhudia ni Meneja Mpya wa Tawi hilo Ndg Mohammed Nuhu anachukua nafasi hiyo ya Meneja wa Tawi hilo la Forodhani Unguja.
 Aliyekuwa Meneja wa Tawi la PBZ Forodhani Ndg. Said Mwinyigkiwa akifurahia wakati wa hafla ya kumuaga baada ya kupata uhamisho kwenda Makao Makuu ya PBZ Zanzibar. Akifurahia baada ya kukabidhiwa keki hiyo na Wafanyakazi wa Tawi hilo wakati wa tafrija ya kumuaga. 
Meneja Mpya wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ Ndg Mohammed Nuhu akiwa na Meneja aliyeagwa na kuhamishiwa Makao Makuu ya PBZ kuchukua Nafasi ya Menaja Masoko PBZ Ndg. Said Mwinyigogo.wakiwa na bashasha wakati wa hafla hiyo.
Wafanyakazi wa PBZ Tawi la Forodhani wakiwa na Meneja wao Mpya Mohammed Nuhu na Meneja wa Zamani Said Mwinyigogo wakiwa na furaha wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Park Forodhani Zanzibar.
Wafanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ wakiwa na Meneja wao wa Zamani Said Mwinyigogo na Meneja wao Mpya Mohammed Nuhu wakikata keki wakati wa hafla hiyo ya kumuaga Meneja wao wa zamani na kumkaribisha Meneja Mpya Mohammed Nuhu. 
Mfanyakazi wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ Tawi la Forodhani Unguja Bi Fahmati Mohammed Bai, akimkabidhi zawadi aliyekuwa Meneja wa PBZ Tawi la Forodhani Unguja Ndg Said Mwinyigogo iliotolewa na Wafanyakazi hayo wakati wa hafla maalum ya kumuaga iliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya ark Forodhani Zanzibar.
Afisa wa PBZ Tawi la Forodhani Said Mussa akitowa maelezo wakati wa hafla hiyo ya tafrija ya kumuaga Meneja wao wa zamani Ndg Said Mwinyigogo na kumkaribisha Meneja Mpya Ndg Mohammed Nuhu.
Afisa wa PBZ Bi. Rashida Mohammed akitowa maelezo ya kumuaga Meneja wao wa zamani Ndg Said Mwinyigogo baada ya kupata uhamisho kwenda Makao Makuu ya PBZ Zanzibar kuchukua nafasi ya Meneja Masoko PBZ na nafasi yake kuchukuliwa na Ndg Mohammed Nuhu.ambae alikuwa ni Meneja Masoko wa PBZ. 
Wafanyakazi wa PBZ Tawi la Forodhani wakifuatilia hafla hiyo ya kumuaga Meneja wao wa zamani Ndg Said Mwinyigogo na kumkaribisha Meneja Mpya Ndg Mohammed Nuhu.Hafla hiyo imefanyika katika hoteli ya Park Forodhani Zanzibar. 

Meneja wa zamani wa PBZ Tawi la Forodhani Ndg Said Mwinyigogo akizungumza na wafanyakazi wa PBZ Tawi la Forodhani wakati wa hafla ya kumuaga ilioandaliwa na wafanyakazi hao, akitowa nasaha zake na kuwataka kudumisha ushirikiano na upendo katika utendaji wa kazi yao ya kila siku wakati wakihudumia wateja wa PBZ na kutowa ushirikiano na Meneja huyo mpya kama walivyokuwa wakitowa ushirikiano wao kwake.
Na kuwatakia kazi njema katika kipindi chao chote cha uongozi huo mpya wa meneja wao huyo Ndg Mohammed Nuhu.
Wafanyakazi wa PBZ Tawi la Forodhani wakifuatilia hafla hiyo ya kumuaga Meneja wao wa zamani Ndg Said Mwinyigogo na kumkaribisha Meneja Mpya Ndg Mohammed Nuhu.Hafla hiyo imefanyika katika hoteli ya Park Forodhani Zanzibar.

Wafanyakazi wa PBZ Tawi la Forodhani wakifuatilia hafla hiyo ya kumuaga Meneja wao wa zamani Ndg Said Mwinyigogo na kumkaribisha Meneja Mpya Ndg Mohammed Nuhu.Hafla hiyo imefanyika katika hoteli ya Park Forodhani Zanzibar.
Meneja Mpya wa Benki ya Watu wa Zanzibar Tawi la Forodhani Ndg. Mohammed Nuhu akizungumza na wafanyakazi hao wakati wa hafla hiyo ya kutambulisha baada ya kuchukua nafasi hiyo katika tawi la Forodhani Zanzibar.
Wakati wa maakuli ya chakula maalum walichowaandalia wakuu wao katika hoteli ya Park Forodhani Zanzibar. 
Meneja Mpya wa Benki ya Watu wa Zanzibar Tawi la Forodhani Ndg Mohammed Nuhu akisoma dua baada ya kumaliza hafla hiyo ya kumuaga Ndg Said Mwinyigogo na kukaribishe yeye kuchukua nafasi hiyo.


Wafanyakazi wa PBZ wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wao baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya kumuaga Meneja wa zamani wa PBZ Tawi la Forodhani Ndg Said Mwinyigogo na kumkaribisha Meneja Mpya wa PBZ Tawi hilo Ndg Mohammed Nuhu. wakiwa nje ya hoteli hiyo ya Park Forodhani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.