Habari za Punde

Watoto ishirini wanusurika kufa Baharini

 
Watoto ishirini wamenusurika kufa wakati wakiwa wanaogelea baharini eneo ya forodhani. 

Watoto hao wanaodaiwa kutoroka chuoni wakati wa asubuhi ambapo polisi jamii wa mji mkongwe wamewaokoa na kuwakamata kuwapeleka katika kituo cha polisi jamii Malindi na baadae kuwapeleka kituo cha polisi Malindi. 

Mkuu wa doria wa Polisi jamii, Issa Omar amesema kumwekuwa na tabia ya watoto kutoka maeneo mbalimbali kufika katika eneo la forodhani kuogelea na wengine kupoteza maisha baada ya kuzidiwa na maji ya bahari. 

Baada ya kusikia taarifa hizo waziri wa elimu na mfunzo ya amali mh. Riziki Pembe Juma amesikitishwa na tukio hilo na kuwataka wazazi kuwafuatilia watoto wao wanapokwenda skuli au madrasa ili kuthibiti matukio kama hayo yasiweze ktokea. 

 Nae mvuvi Shemata Masoud mara nyingi wanapokuwa katika shughuli zao uvuvi huwa wanawaokoa watoto tofauti na kufurahi kuwa baada ya watoto hao kuokolewa. 

Zbc haikuishia hapo ilifika katika kituo cha polisi Malindi ambapo watoto hao wamehifadhiwa kwa usalama zaidi hivyo kila mwenye mzazi amabe mtotio wake hamuoni afike kituoni hapo kwa maelezo zaidi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.