Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Azungumza na Wakuu wa Vyombo Vya Habari na Wahariri Kuhusu Uzinduzi wa Mimi na Wewe.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mohmoud akizungumza na Wakuu wa Vyombo vya Habari Zanzibar adhma yake ya kuadhimisha mwaka mmoja wa kuchaguali kwake kushika nafasi hiyo kwa Uzinduzi wa Mpango wa kuinua hali za Wananchi wa Mkoa wake kwa Kampeni ya Mimi na Wewe. Kwa Matembezi na Uchangiaji wa Damu katika viwanja vya Bustani ya Mnara wa Kumbukumbu Michezani siku ya tarehe 21, Mei 2017.   
Mradi wa Kampeni ya Uzinduzi huo wa Mimi na Wewe Ndg. Mohammed Nuhu akifafanua jambo wakati wa mkutano huo wa kutowa taarifa kuhusu madhmuni yake Mpango huo wa Mimi na Wewe kujenga maandili ya Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi na Wananchi wa Zanzibar kwa kufanuikisha mpango huo.   
Mkurugenzi Mkuu wa Zenj FM Mhe Mohammed Seif Khati akichangia wakati wa mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Vuga Unguja.
Mkuu wa Chuo cha Waandishi MCC Ndg. Suleiman Seif akichangia wakati wa mkutano huo. 
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja akifafanua jambo wakati wa mkutano wake na Wakuu wa Vyombo vya Habari Zanzibar vya Serikali na Binafsi juu ya Mpango wake wa kuzindua Mimi na Wewe. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.