Habari za Punde

Spika BLW amuapisha Mhe Ahmada Yahya Abdulwakil kuwa Mjumbe wa baraza la wawakilishi

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zubeir Ali Maulid akimuapisha Mhe. Ahmada Yahya Abdulwakil kuwa mjumbe wa BLW huko Chukwani leo
Mjumbe wa Baraza la wawakilishi kuteuliwa Nafasi za Rais Mhe Ahmada Yahya Abdulwakil akitia saini hati za uapisho baada ya kuapishwa kuwa mjumbe wa baraza la wawakilishi hivi leo
Mjumbe wa Baraza la wawakilishi Mhe Ahmada Yahya Abdulwakil akiwa katika kiti chake tayari kutekeleza majukumu yake ya uwakilishi

Spika wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid amemuapisha Ndugu Ahmada Yahya Abdulwakil kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na kulifanya Baraza hilo kuwa na idadi ya wajumbe 87 hivi sasa.


Mheshimiwa Ahmada ameteuliwa Mei 15 Mwaka huu na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dkt Ali Mohamed Shein kupitia uwezo wake wa Kikatiba. 

Uteuzi huo ameufanya kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 66 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Kifungu hicho kinampa uwezo wa kuchagua watu kumi wenye sifa za kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na hadi hivi sasa tayari ameshatumia nafasi tisa.

Mchanganuo kamili ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi hadi hivi sasa ni kama ifuatavyo.

1. Wajumbe wa kuchanguliwa kutoka majimboni = 54

2. Wajumbe wa Kuteuliwa na Rais wa Zanzibar = 9
3. Wajumbe wa VIti Maalum vya Wanawake = 22
4. Mwanasheria Mkuu = 1
5. Spika = 1
Jumla = 87

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.