Habari za Punde

Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd.(PBZ) Yakabidhi Msaada wa Vyakula Kwa Vituo Vya Watoto Yatima Zanzibar.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Juma Ameir akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali wakati wa zoezi la kukabidhi msaada kwa Vituo vya Watoto Yatima Zanzibar ili kuweza kufurahia mwenzi Mtukufu wa Ramadhani na Kusherehekea Sikukuu ya Iddi baada ya mfungo huu ramadhani ili kuweza kujumuiya na wananchi wengi katika hali ya furaha jumla ya vituo sita vya Watoto yatima unguja vimepata msaada huo uliotolewa na PBZ kupitia benki ya Islamic.  
Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Said Ali Mwinyigogo akimkabidhi mmoja wa mtoto katika kituo cha Watoto Yatima cha Mazizini Zanzibar (zamani kikijulikana kwa jina la forodhani) Salma Abdallah Ali akishuhudia Mkuu wa Kituo hicho Bi Saada Ali Mohammed, hafla hiyo imefanyika katika makaazi yao mazizini Unguja
Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini wakiwa katika hali ya furaha baada ya kukabidhiwa msaada wa vyakula Unguja wa Ngano, Mchele, Sukari na Mafuta ya kupikia kwa ajili ya mfungo wa mwezi wa Ramadhani na Sikukuu ya Iddi Fitry inayotarajiwa kusherehekewa baada ya mfungo kumalizika.
Mkuu wa Kituo cha Watoto Yatima Mazizini Zanzibar Bi Saida Ali Mohammed akitowa shukrani kwa Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa msaada wao huo umefika wakati muafaka na utatumika kama uliovyokusudiwa na kuwataka wafanyabiashara kujitokeza kusaidi katika vituo vya Watoto Yatima Zanzibar. ili kuiga mfano wa PBZ kujali jamii ya Wananchi wa Zanzibar.  
Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar wakiwa na furaha baada ya kupokea msaada huo wa vyakula uliotolewa na Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ kwa ajili yao kuungano na watoto wenzao katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuweza kusherehekea Sikukuu ya Iddi Fitry kwa uzuri.

Mkurugenzi wa Masoko wa PBZ Ndg. Saili Ali Mwinyigogo akiwakabidhi msaada wa Vyakula Watoto wa Kijiji cha SOS Mombasa Zanzibar watoto Halfan Khamis na Talali Suleiman. Mkurugenzi wa Masoko wa PBZ Ndg Said Mwinyigogo akimkabidhi Mlezi Mkuu wa Kituo cha Watoto Yatima cha Islamic Center Mombasa kwa Mchina Bi Zalha Abdallah kwa ajili ya Kituo hicho. 
Mkurugenzi wa Masoko PBZ Ndg Said Ali Mwinyigogo akimkabidhi msaada wa vyakula Amiri wa Kituo cha Watoto Yatima cha Fisabilily Tabliy Markaz Fuoni Zanzibar  Amiri Mkubwa Ali. 

Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd Ndg. Said Ali Mwinyigogo akikabidhi msaada wa Chakula kwa Watoto wa Kituo cha Watoto Yatima cha Motsseori Bububu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.