Habari za Punde

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Shein Aweka Jiwe la Msingi Tawi la CCM Unguja Ukuu Kae Bona.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Unguja Ukuu Kae Bona wakati wa hafla ya kuweka jiwe la Msingi la Tawi la CCM KaeBona Unguja Ukuu, akiwa katika ziara yake kutembelea Mkoa wa Kusini Unguja na kuimarisha Chama, kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhani Ali Kichupa Mbunge wa Jimbo la Tunguu Mhe Khalifa (Mimina) na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe Simai Mohammed Said (MpakaBasi) wakifuatilia uzinduzi wa uwekaji wa jiwe la msingi la Tawi hilo lilioko katika jimbo lao.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la CCM Unguja Ukuu Kae Bona Wilaya ya Kati Unguja akiwa katika ziara yake Mkoa huo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, na Viongozi wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja wakipiga makofi baada ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Tawi la CCM Unguja Ukuu KaeBona.  
Mwenyekiti wa Tawi la CCM Unguja Ukuu Kae Bona Ndg. Khatibu Ramadhani kulia akitowa maelezo kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, baada ya kuweka jiwe la msingi na kutembelea ujenzi wa Tawi hilo la kisasa likiwa na vitega uchumi baada ya kukamilika ujenzi wake. 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhani Ali Kichupa akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCN Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi kumkaribidha Dk Shein.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Tawi la CCM Unguja Ukuu kae bona wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein Mkoa wa Kusini Unguja.
Wananchi wa Kijiji cha Unguja Ukuu Kaebona wakifuatilia hafla hiyo. ya uwekaji wa jiwe la msingi la Tawi lao la CCM. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.