Habari za Punde

Coco Sports Ndondo Cup 16 Bora Kuanza Kesho Kutwa Jumanne na Kutolewa Ratiba Kamili ya Michuano Hiyo.

Na: Abubakar Khatib Kisandu..
Mashindano ya Soka ya Coco Sports Ndondo CUP yamefikia hatua ya timu 16 bora mtoano ambapo awali Ndondo hiyo ilianza na timu 63 kwa kuchezwa mtoano na mpaka sasa kufikia hatua ya 16 bora pia hatua hiyo itachezwa kwa mtoano.

Timu 16 zilizofanikiwa kutinga hatua hiyo ya 16 bora ni Six Center, Meli 10 City, Real Nine, Kibondemaji, Amazon, Mafia, Theo Kombain, Raskazone, Usitetemeke, Bilbao, Mahonda Kombain, Lakidatu, Blue Star, Chumbuni Cotex, Taifa ya Donge pamoja na G-Unity. 

Michezo hiyo yote itapigwa katika uwanja wa Blue Star Mwera kuanzia saa 10:00 za jioni ambapo mchezo wa kwanza utaanza kati ya Six Center ya Mwera dhidi ya Meli 10 City ya Kama mchezo ambao utapigwa kesho kutwa Jumanne Septemba 5, 2017.

Mashindano hayo yameandaliwa na kituo cha Radio cha Coconut FM 88.9 kupitia kipindi chake cha Michezo cha Coco sports ambapo bingwa anatarajiwa kupatiwa Ng'ombe na Shilingi Milioni moja.

RATIBA KAMILI HII HAPA
Jumanne 5/9/2017 Six Center v/s Meli 10 City
Jumatano 6/9/2017 Real Nine v/s Kibondemaji
Alhamis 7/9/2017 Amazon v/s Mafia
Ijumaa 8/9/2017 Theo Kombain v/s Raskazone
Jumapili 10/9/2017 Usitetemeke ya Tumbatu v/s Bilbao
Jumatatu 11/9/2017 Mahonda Kombain v/s Lakidatu
Jumanne 12/9/2017 Blue Star v/s Chumbuni Cotex
Jumatano 13/9/2017 Taifa ya Donge v/s G Unity.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.