Habari za Punde

Jeshi la Polisi Kisiwani Pemba Lamshikilia Kijana Kwa Tuhuma za Biashara ya Dawa za Kulevya.

Na Masanja Mabula - Pemba

Katika mwendelezo wa operesheni wa utokomezaji wa madawa ya kulevya wa Jeshi la Polisi nchini hatimae Jeshi hilo mkoa wa Kusini Pemba jana limefanikiwa kumkamata  kijana mwengine akiwa na jumla ya kete 241 zinazodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kamanda wa polisi mkoa wa kusini Pemba  Shekhan Mohammed Shekhan amemtaja kijana waliyemkamata kuwa ni Haji Balozi Hassan (35) ambae alikuwa kwenye gari ya abiria akitokea  mkoani kuelekea micheweni.

Alisema katika gari hiyo askari walimtilia mashaka abiria huyo ndipo walipoamua kumpekua na kufanikiwa kumkamata na madawa hayo aliyokua nayo katika mifuko yake ya suruali.

" Mpaka hivi sasa yupo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi na leo tutampeleka mahakamani kusomewa kosa lake" alisema Kamanda Shehan

Kamanda Shehan ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi ili kufanikisha kutokomeza madawa ya kulevya yanayoonekana kuwa ni tatizo katika jamii.

Tukio la kukamatwa Hassan  ni tukio mfululizo wa watuhumiwa wa madawa hayo kukamatwa kisiwani Pemba  ambapo juzi Jeshi hilo lilifanikiwa kumtia mikononi mwanamke mmoja mkaazi wa Wete akiwa na kete 3621 zinazodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya katika maeneo ya mbuguani Mkoani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.