Habari za Punde

Ratiba ya Nusu Fainali Ndondo Cup yatolewa

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kamati inayosimamia Mashindano ya Coco Sports Ndondo Cup leo imetangaza ratiba ya nusu fainali ya mwaka 2017.


Hii ndio nusu fainali ya COCO SPORTS NDONDO CUP 2017


Jumapili 24/9/2017
Theo Kombain vs Kibonde Maji

Jumatatu 25/9/2017
Six center vs Amazon fc
Mechi zote zitapigwa katika uwanja wa blue star Mwera saa 10: 00 za jioni.

Mashindano hayo ya Ndondo CUP awali yalianza na timu 63 kwa kuchezwa mtoano na mpaka sasa kufikia hatua ya nusu fainali  ambapo bingwa anatarajiwa kupatiwa Ng'ombe na Shilingi Milioni moja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.