Habari za Punde

Wadau wa Elimu Watoka na Maadhimio ya Changamoto na Mafanikio ya Elimu.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe akitoa hotuba wakati akifunga kikao cha pamoja kati ya Wadau wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma leo. 
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Sylvia Temu akitoa maelezo ya awali kuhusu kikao cha Wadau kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Mkuu OR TAMISEMI wakati wa kufunga kikao cha Wadau wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma leo 
Mwakilishi wa Wadau wote wa Maendeleo nchini Tanzania (toka Uingereza - DfID) Bi.Janeth Tanya akitoa maelezo mafupi kwa niaba ya Wadau kabla ya ufungaji wa kikao kati ya  Wadau wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma leo 
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu Bw. Tixion Nzunda akitoa maelezo ya awali kabla ya hotuba ya Mgeni Rasmi Katibu Mkuu OR TAMISEMI wakati wa kufunga kikao cha Wadau wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma leo.
Mwakilishi wa Wanafunzi, Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Dodoma Manispaa darasa la sita Sylvester Allen akipeana mikono na Mgeni Rasmi wakati wa ufunguji wa kikao kati ya  Wadau wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma leo 
Baadhi ya Washiriki walioshiriki kikao cha kikao cha Wadau wa Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma leo 

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Eng. Musa Iyombe amesema Serikali itahakikisha inatekeleza maazimio yote yaliyopitishwa kwenye Mkutano wa pamoja wa mwaka wa wadau wa Elimu uliofanyika kwa siku nne Mjini Dodoma.
Eng. Iyombe ameyasema hayo wakati wa kufunga Mkutano wa mwaka wa wadau wa Elimu wenye lengo la kujadili changamoto, mafanikio ya Elimu na kuona namna gani kama wadau wanaweza kutafuta njia ya pamoja ya kuboresha Mfumo wa utoaji wa Elimu Tanzania.

“Nimepokea maazimio yote ya Mkutano huu na ntayawasilisha panapo husika kwa ajili ya Utekelezaji lakini pia niwapongeze kwa kazi kubwa mliofanya, kuanzia wataalamu kutoka Serikalini, sekta binafsi, Mashirika yasiyo ya kiserikali, wadau wa Elimu hakika mmefanya kazi kubwa na kupitia Mkutano huu tutaona mabadiliko makubwa katika Sekta hii ya Elimu” alisema Iyombe.


Akitoa salamu za Wizara Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof sylivia Temu amesema Kikao kimekuwa na tija kwa kuwa pamoja na mambo mengine kimejadili masuala ya nayotokana na utafiti wa elimu na kwamba matokeo yatafit iyaliyoonyesha changamoto yatafanyiwa kazi kwa pamoja kati ya serikali, wadau wamaendeleo na mashirika yasiyo ya serikali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.