Habari za Punde

Ligi Kuu ya Zanzibar Kati ya JKU na Taifa ya Jangombe Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu Hizo Zimetoka Sare ya Bila Kufungana.

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Jangombe wakiwa katika benchi la ufundi wakifuatilia mchezo wao na Timu ya JKU mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana. 
Mchezaji wa Timu ya JKU kushoto Shomar Waziri na mchezaji wa Timu ya Taifa ya Jangombe Abdillah Abdallah wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana. 
Mshambuliaji wa Timu ya JKU Almas Said akijiandaa kuzuiya mpira huku beki wa Timu ya Taifa ya Jangombe akijaribu kumzuiwa wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Amaan. 
Beki wa Timu ya Taifa ya Jangombe akiruka juu kuokoa mpira golini kwao. 
Wachezaji wa Timu za JKU na Taifa ya Jangombe wakipata maelekezo kutoka kwa makocha wao wakati wa mmoja wa mchezaji wa Timu ya JKU akipata huduma ya kwanza baada ya kuumia mchezoni.
Mshambuliaji wa Timu ya JKU Almas Said akimpita beki wa Timu ya Taifa ya Jangombe Abdillah Abdallah wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar. timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana. 
Mshambuliaji wa Timu ya JKU Issa Haidar akimpita beki wa Timu ya Taifa ya Jangombe Nabil Mussa. 
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Jangombe Abdallah Mudathir akimpita beki wa Timu ya JKU Issa Haidar wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.