Habari za Punde

Waziri Makamba akutana na uongozi wa Jumuiya ya wafanyabiashara Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba akizungumza na wanajumuiya ya Wafanyabiashara wa Zanzibar (hawapo pichani). Kikao hicho kimefanyika eneo la Kinazini Zanzibar. Wengine katika picha ni viongozi wa Jumuiya hiyo.
Sehemu ya wafanyabiashara wa Zanzibar wanaounda Jumuiya ya Wafanya Biashara wa Zanzibar wakiwa katika kikao na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba aliyewaalika kujumuika kubadilishana uzoefu na kuwaomba waainishe changamoto zinazowakabili na kuona namna bora ya kuzipatia ufumbuzi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba akisalimiana na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano katika Serikali ya awamu ya nne Mhe. Mohammed Seif Khatibu ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Zanzibar Media Coorporation, Waziri Makamba alipata pia wasaa wa kufanya mahojiano katika chombo cha Habari cha Zenji FM na Zenji TV.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba akifanya mahojiano maalumu katika Kituo cha Redio cha Cocunut FM. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba ameanza ziara ya kikazi ya siku saba visiwani Zanzibar. Katika siku ya kwanza Mhe. Makamba amepata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Zanzibar kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kubaini fursa na changamoto zinazowakabili na kuona namna bora ya kupata ufumbuzi.

Miongoni mwa changamoto zilizojadiliwa na kuwekewa mikakati ya utekelezaji ni pamoja na masuala ya kodi, namna ya kunufaika kutoka na fursa zilizopo baina ya pande zote mbili za Muungano na kuondoa vikwazo vinavyotokana na changamoto hizo ili kuleta ufanisi.

Mhe. Makamba amewahakikishia wana juimuiya hao kuwa Ofisi yake itaratibu vikao kati ya Ofisi yake na wafanyabiashara hao ili kupata fursa ya kutoa mrejesho wa utekelezaji wa mambo waliyokubaliana.

Mbali ya kukutana na wafanyabiashara hao Waziri Makamba pia amepata fursa ya kutembelea Vyombo mbalimbali vya Habari hapa Unguja kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya Muungano. Vyombo vilivyotembelewa ni pamoja na Zenji FM na Zenji Tv, Bahari FM na Cocunut FM.

Ziara ya Waziri Makamba katika siku pili atatembelea Miradi mikubwa ya Mazingira na kuwa na Vikao na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRB)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.