Habari za Punde

Amour Pwina aibeba Zanzibar Heroes


Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) imeendelea kucheza michezo ya kirafiki ambapo leo imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 baada ya kuifunga timu ya Kombain iliochaguliwa na Makocha wa Zanzibar, mchezo wa kirafiki uliopigwa saa10 jioni katika uwanja wa Amaan.

Mabao ya Heroes yote yamefungwa na Amour Suleiman (Pwina) dakika ya 35 na 80 ya mchezo.

Huu ni mchezo wa tano wa kirafiki kwa Heroes kufuatia awali kutoka sare ya bao 1-1 na Kombain ya Unguja, kisha wakatoka tena sare ya 1-1 na Taifa ya Jang'ombe, wakaifunga Villa United 5-2, jana wakaichapa Dulla Boys 2-1 na leo kushinda 2-0.

Kwasasa Heroes watacheza mchezo mmoja tu wa kirafiki kabla ya kuelekea Kenya katika Mashindano ya CECAFA ambapo mchezo wao wa mwisho wa kujipima nguvu utapigwa siku ya Jumanne saa 11:00 za jioni katika uwanja wa Amaan dhidi ya Kombain ya Wachezaji wanaocheza ligi kuu soka Tanzania Bara ambao hawakuitwa Heroes.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.