SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
WIZARA YA
HABARI UTAMADUNI UTALII NA MICHEZO
Tel: 0255 24 2237325/0255 24 223 7313 Idara
ya Habari Maelezo
Fax: 0255 24 2237314 P.O.Box
2754
E-mail:habarimaelezo@yahoo.co.uk, maelezozanzibar@zanlink.com Zanzibar
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Meli
inayofanya utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia ya MV. BGP EXPLORER ya China leo
itakuwa katika maeneo ya karibu sana na Mwambao wa Kisiwa cha Pemba wakitokea
Kusini Magharibi ya Kisiwa hicho.
Kwa
saa 38 zijazo, Meli hiyo ya Utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia kwa njia ya
Mitetemo Baharini ikifanya utafiti eneo lote la Pwani ya Magharibi ya Kisiwa
cha Pemba na hivyo Meli itakuwa ikitembea karibu sana na Kisiwa.
Hadi
kufikia jana, Watafiti hao wametafiti njia 14 licha ya Mvua kubwa inayoendelea
kunyesha ambapo pia wamekumbana na ukungu katika Pwani ya Kusini Magharibi ya
Kisiwa cha Pemba.
Serikali
inawaomba wananchi wasiwe na wasiwasi watakapoiona Meli hiyo ambayo kwa sasa
itakuwa ikitembea karibu sana na Kisiwa.
Mamlaka
ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta Zanzibar(ZPRA) inawaomba radhi
Wavuvi kwa usumbufu unaojitokeza hasa pale wanapolazimika kusubiri kwa saa
kadhaa kupisha shughuli za utafiti wakati Meli inapopita karibu na maeneo ya
uvuvi.
ZPRA
inawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano katika zoezi hili na
inawashukuru kwa ushirikiano wao wanaoutoa wakati wote wa zoezi la Mitetemo Baharini.
Imetolewa
na :
Dk. Juma Mohammed Salum
K.N.Y
Mkurugenzi
Idara ya Habari(MAELEZO) Zanzibar
05, Novemba, 2017
No comments:
Post a Comment