Habari za Punde

Sailors yachapwa na Zimamoto, Boys waanza Ligi


Kikosi cha Black Sailors

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja imeendelea tena jana kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan ambapo saa 8 za mchana Jang'ombe Boys waliichapa Charawe mabao 4-2.

Mabao ya Boys yamefungwa na Khamis Mussa (Rais) dakika ya 3, 9, na 21 (Hat-trick) na bao la nne likifungwa na Hafidh Bariki (Fii) dakika ya 83 huku mabao ya Charawe yakiwekwa nyavuni na Ulimwengu Edimundi dakika ya 66 na Yussuf Mkubwa dakika ya 68.

Saa 10 za Jioni Black Sailors ikachezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Zimamoto.

Mabao ya Zimamoto yamefungwa na Hamid Mgeni dakika ya 45 na Juma Ali dakika 80 huku bao pekee la Sailors likifungwa na Hassan Mkwabi dakika 78.

Ligi hiyo kesho itakwenda mapumziko na itaendelea tena Jumatatu ya Novemba 6 katika uwanja wa Amaan ambapo Saa 8:00 za mchana Polisi dhidi ya KMMK na saa 10:00 za jioni Kilimani City dhidi ya Chuoni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.