Habari za Punde

Wazanzibari walioitwa Timu ya Taifa ya Tanzaniia U/23 waenda kambini leo

Wachezaji Mohammed Jailan Habibu  kulia na Faisal Salum wakiwa Bandarini kuelekea Dar

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kiungo wa Miembeni City Mohd Jailan Habibu na Fesal Salum wa JKU leo wameondoka Zanzibar na kuelekea Tanzania Bara katika Kambi ya timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 23 maarufu kwa jina la Kilimanjaro Warriors.

Benchi la Ufundi la timu za taifa za vijana, limeita wachezaji 35 kwa ajili ya kambi yenye lengo la mchujo kutafuta kikosi imara cha timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 23 ambapo miongoni mwa wachezaji hao wawili wanatoka ligi ya Zanzibar ambao ni Wazanzibar.

Kocha Msaidizi wa timu hizo, Oscar Mirambo alitangaza majina hayo Juzi Novemba 03, mwaka huu huku akisema wanahitaji vijana wasiozidi 25 kwenye kikosi ambao leo Jumapili wameanza kambi ya siku 10.

Wachezaji aliowaita ni makipa Metacha Mnata (Azam FC), Joseph Ilunda (JKT Ruvu), Liza Mwafwea (Tanzania Prisons).
Wengine ni Cleotas Sospter (Yanga); Idrissa Mohammed, Bakari Kijuji (Yanga), Joseph Prosper (Azam), Masoud Abdallah (Azam), William (Ruvu Shooting), Yussuph Mhilu (Yanga), Adam Salamba (Stand United), Omary Mponda (Ndanda) na Stanley Angeso (Stand United).

Pia wamo Eliud Ambokire (Mbeya City), Emmanuel Kakuti (Mbeya City), Medson Mwakatunde (Mbeya City), Daruweshi Shaliboko (Ashanti Unted), Abbas Kapombe (Azam/Ndanda), Ismail Aidan (Mtibwa Sugar), Salum Kihimbwa (Mtibwa Sugar), Hassan Mganga (Mtibwa Sugar) na Award Salum (Njombe Mji).


Wengine Awesu Ally (Mwadui), Salum Chuku (Singida United), Yahya Zayd (Azam), Emmanuel Martin (Yanga), Geofrey Mwashiuya (Yanga), Ayoub Masoud (Ndanda), Baraka Majogoro (Ndanda), Mohammed Habib (Miembeni city), Yussuf Mlipili (Simba), Agathon Mapunda (Njombe Mji), Faisal Abdallah (JKU) na Yussuph Kagoma (Singida United).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.